Friday, April 3, 2015

ZIJUE TOFAUTI KATI YA INJILI YA KIMISSIONARY NA INJILI YA KIFALME NA APOSTLE VINCENT MAKALLA
Mtumishi wa Mungu Apostle Vincent Makalla ambae ni kiongozi wa kanisa la Victory Faith lililopo Arusha amefundisha tofauti kubwa iliyopo kati ya injili ya kifalme na injili ya kimissionary, na akafundisha kuwa ukiijua injili ya kifalme hautakuwa na manung'uniko katikautumishi wako. Apostle Makalla amesema
Picha ya kanisa la Victory Faith kwa nnje
"Yesu alisema kabla ya mwisho Gospel of king dom itahubiriwa. sasa hii injili ya ufalme inataka ihubiriwe na watu wenye Rank ya kifalme Muh10:15, Na huwezi kuongea juu ya ufalme bila fedha. Wanao subiri bahasha ndipo waka hubiri nisawa lakini hiyo ni injili ya ki missionary hiyo unangoja watoe ndipo uende. hiyo ilisha pitwa na wakati. Ufeso 5:10, Watumishi wa Mungu tuna paswa kuwa sawa na hili andiko. Ufalme na ukuhani. Yaani Makuhani 100% na Watawala matajiri100%, wakati mwingine watumishi wana dharauliwa sio kwasababu ya huduma bali ni ufukara uliyo kithiri." Apostle Makalla ambae mbali na huduma lakini anajishughulisha na biashara mbalimbali halali amesisitiza kuwa ni vyema kwa watumishi tuliopo katia karne hii kujifunza misingi ya injili ya kifalme ambayo utendaji wake unaleta heshima katika nyumba ya Mungu.
Apostle Makalla akiwa anafundisha katika
Apostle Makalla ambae siku za nyuma alipost ujumbe kwenye facebook unaosema unaweza kukataa kuwa mzigo ni jambo la muhimu sana..

No comments:

Post a Comment