Saturday, April 4, 2015

Mjumbe wa Mapenzi ya Mungu Eliya Ad2 Mungu wa Majeshi hajafa bali kuna sehemu amejificha.

Ni miezi kadhaa imekatika tangu Mchungaji kiongozi wa kanisa la Pool Of Siloam kufariki dunia huku kila mtu akibakia na nenolake la kusema. Wengi walitukana na kuikashifu imani yake huku wengine wakiendeleakuamini bila kuyumbishwa na maneno. Wakati bado mambo hayajapoa sawasawa na stori za Eliya zikiwa bado ziko vinywani mwa wengi katika hali ya uzuri na wengine hali ya ubaya, Mtumishi wa Mungu Bishop Nickodemus Shaboka ambae ni mchungaji msaidizi katikakanisa la Citty Harvest international lililopo Posta Mpya ameibuka na kutoa mpya kuhusu kifo cha Eliya.
Mchungaji Nikodemus Shaboka amesema kwamba kwa hisia zake bado hajaamini sana kama huyuMtumishi amekufa, bali anangojea muda upite ndipo aamini, maana Eliya alikuwa ni mtumishi mwenye mafunuo mapya kila kukicha ambayo hayaeleweki, kama aliweza kujihisi yeye ni Mungu kwa makusudi yake binafsi, Hawezi kushindwa kujificha mahali na kuzusha amekufa ili siku moja aje atokee ghafla na kuzusha kuwa amefufuka kama Yesu. Ila kama ni kweli amekufa basi Mungu amuweke pale anapostahii kuwa..

No comments:

Post a Comment