ALIYEMSHTAKI ASKOFU GWAJIMA AFAHAMIKA
Hatimaye imefahamika kuwa mwananchi anayejulikana kwa jina la Abubakar
Yusufu, mkazi wa Kiluvia wilaya ya Kisarawe, ndiye aliyefungua kesi
polisi akilalamika kukwazwa na lugha iliyotumika na Askofu Gwajima dhidi
ya Askofu Mkuu Kanisa Katoliki jimbo kuu la Dar es Slaam, Kardinali
Pengo.
Jana polisi walipanga kuendelea kumhoji Askofu Gwajima
hata hivyo walilazimika kuahirisha mahojiano hadi tarehe 9-Aprili
kufuatia hali ya Gwajima kutokuwa ya kuridhisha.
Askofu Gwajima
alifika kituo cha Polisi cha Kati akiwa katika baiskeli ya kusukumia
wagonjwa ambapo kutokana na hali yake kiafya kutokuwa nzuri alishindwa
hata kupandisha ngazi.
No comments:
Post a Comment