Mwaka 2007 kanisa la Calvary Asemblies Of God (chuo cha manabii) waliandaa semina ya wiki nzima, ambapo katika semina hiyo wanenaji walikuwa ni Apostle John Sekalala, Apostle Chriss pamoja na Apostle Dansan Maboya. Semina hiyo ilikuwa ni moto wa kuotea mbali. Nilibahatika kuhudhuria semina hiyo kwa muda wote iliyoendela na kwakweli kuanzia hapo maisha yangu kitumishi yalianza kupata ongezeko.
Siku moja nilipokuwa kwenye semina hiyo alisimama Apostle Maboya na kuanza kufundisha somo ambalo alilipa Title ya Kuvuna ulichokipanda. Andiko alilosimamia ni andiko la kawaida sana ambalo tumelizowea toka (Wagalatia 6:7 Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi; kwa kuwa cho chote apandacho mtu, ndicho atakachovuna.) baada ya hapo akaendelea kufundisha kwa kusema kuwa siku zote wakati mtu anapanda mbegu ya uovu utakuta yeye mwenyewe anafurahia, na wala hawezi kuona tatizo kwasababu ule uovu anaoufanya inawezekana ukawa unamsaidia kwa muda ule na yeye mwenyewe akaona hana njia nyingine zaidi ya hiyo. Apostle Maboya akatolea mfano wa Yakobo na kusema wakati Yakobo anamdanganya baba yake yeye akilini mwake alikuwa anawazia kupata baraka tu, lakini hakujua ule uongo aliomdanganya baba yake utakuja kumgharimu mbeleni. Miaka mingi baadae wakati yeye amesha sahau na tena amesharekebisha tofauti yake na kaka yake Esau, Uongo ule ule aliomdanganya baba yake na yeye watoto wake walikuja kumdanganya tena kwa uongo mkubwa zaidi.
Yeye alidanganya tu na kuchukua baraka za Esau, lakini wanae wakamdanganya kuwa Yusufu kararuliwa na mnyama mkali na kufa, machozi aliyolia Esau na yeye alilia kwa uchungu uleule tena inawezekana zaidi ya ule na tena kwa machozi yaleyale. Zaidi yeye akaweka msiba na kuomboleza kwa siku kadhaa akimuombolezea mtu ambae yuko hai. Hii inaweza kuonekana kawaida lakini Yakobo alikuwa analipa gharama za uongo aliomdanganya baba yake miaka mingi iliyopita pamoja na machozi aliyomliza kaka yake. Ni kweli Esau alisamehe lakini kanuni za Mungu hazikubadirika juu ya kumlipa kile alichokipanda... Yatafakari hayo..
No comments:
Post a Comment