Chama cha upinzani cha APC kimeshinda nigeria.
Nadhani sasa
chama kilichokuwa tawala na sasa cha upinzani cha PDP kinachoongozwa na
rais aliyeangushwa Goodluck Jonathan kimejifunza kitu baada ya
kuangushwa.
Chama tawala nchini nigeria cha peoples democratic
part (PDP) kimeangushhwa kwenye uchaguzi wa jumamosi na chama cha All
Progressives Congress (APC) kinachoongozwa na Muhammadu Buhari.
Viongozi wa PDP akiwemo rais jonathan walikuwa wanafanya siasa kama za
chama tawala tanzania ccm.kila kukicha walikuwa bize namna ya
kudhoofisha wapinzani na kujikuta wakisahau majukumu yao wakiwa kama
chama tawala wakati huo mapigano ya boko haram na jeshi la nchi
yakiendelea na watu wasiokuwa na hatia wakiendelea kuuwawa,
Kitendo cha siasa za majungu na kutafutiana visa chama tawala zidi ya
upinzani kilimkera sana muasisi wa chama hicho na rais mstaafu wa
nigeria bwana Olusegun Obasanjo.muasisi huyo aliweza kumuhoji rais
jonathani kuwa wapi mnakipeleka chama?Lakini kama mnavyojua sikio la
kufa halisikii dawa na MUNGU atapotaka kuupoka utawala madaraka huupiga
upofu.viongozi wa wa PDP akiwemo rais jonathani walimkashifu na
kumtukana muasisi huyo bwana obasanjo kitendo kilichomfanya obasanjo
kuchana kadi ya uanachama na kujitoa kwenye chama hicho ijapo wao PDP
wanadai walimtimua.
No comments:
Post a Comment