Jeshi la Polisi Kanda
Maalum DAR limesema wafuasi wa Askofu Gwajima ni marufuku kutia mguu
eneo atakalohojiwa Askofu huyo, ambapo kauli hiyo imekuja siku chache
baada ya Askofu huyo kuwataka wafuasi hao kumsindikiza kuelekea kituoni
hapo.
“Napenda kutumia nafasi hii
kumuomba GWAJIMA awaambie wafuasi wake hawahitajiki kufika eneo hilo..
anayehitajika ni yeye na Mwanasheria wake”—Kamanda Suleiman Kova.
Kamanda Kova amesema iwapo kila mtu atafuata taratibu hakuna nguvu itakayotumika.
No comments:
Post a Comment