Katika utoto wangu na hadi sasa ni kijana ninaeuelekea utu uzima nimekuwa nikisikia sana jina la Father Nkwella likitajwa na watu wengi, wakatoliki na na wakristo wasio wakatoliki. Wapo waliomuongelea kwa uzuri na wengine kumuongelea kwa ubaya, lakini katika miaka yote sijawahi kubahatia kumuona live Father Nkwella na hata kanisa lake sijui liko sehemu gani. Kwa bahati mbaya nilipata msiba siku ya ijumaa ambapo mazishi yalifanyika siku ya jumanne ya tar 12/April/2015 ambapo katika msiba huo Father Nkwella alihudhuria kwasababu marehemu alikuwa ni rafiki yake wa karibu sana na muumini wake. Baada ya mazishi kufanyika kuna mtu alinishtua kuwa yule unaemuona mbele yetu unamjua? Nikamjibu simfahamu, akaniambia kama umewahi kusikia mtumishi anaeitwa Father Nkwella ndio huyo. Aliponiambia hivyo nikasema siwezi kuondoka na kuishia kumuona kwa mbali ngoja nikamuombe angarau nipige nae picha, ingawa alikuwa amezungukwa na watu wengi lakini nilifanikiwa kupenya na kumfikia, nikakaa pembeni yake kwa muda wa dakika 10 na alipomaliza kuongea na watu ndio nikamumpa mkono na kumsalimia. Alipoitikia salamu yangu nikaonyesha jinsi nilivyofurahi kuonana nae na nikamuomba kupiga nae picha, hakuonyesha kusita akakubali mara moja, wakati tumemaliza kupiga picha niamuuliza kwa sauti ya chini chini, "Kanisa lako kwa chalinze liko wapi? Akanijibu hana tawi chalinze ila taratibu taratibu tu mambo yatakuwa. Nikamuuliza tena kwanini watu hasa jamii ya wakatoliki wenzake wanamuongelea vibaya na kufikia hadi hatua ya kuwanyima sakramenti waumini wake? Akanijibu, huduma yeyote ya kweli lazima ikutane na vita pamoja na kukataliwa na hiyo ndio tafsiri sahihi ya kukinywea kikombe cha Kristo. Swali la mwisho nikamuuliza je, yeye anatofauti gani na wakristo waliookoka? Na kwanini asijiite mchungaji yeye anajiita Father? Akanijibu eneo tulilopo sio sahihi sana kwa kujadiri mambo hayo ila nikihitaji kujua mengi ananikaribisha kanisani ubungo. Baada ya kunijibu hayo kwa njia ya hekima na upole kabisa niliona kweli nimuache kwanza mzee aendelee na majukumu mengine lakini nimepanga kumtafuta ili nimuulize mambo mengi sana kuhusiana na huduma yake.
|
Father Nkwella akiwa anapeana mkono wa salamu na Mjane wa Marehemu |
|
|
Father Nkwella akizungumza na Mjane wa Marehemu |
|
Father Nkwella akiwa amezungukwa na familia ya marehemu |
No comments:
Post a Comment