Monday, April 6, 2015

JUMUIYA YA WAKRISTO YAMUARIKA PROFESA JAY KUWA MGENI RASMI KATIKA TAMASHA LA PASAKA LILILOFANYIKIA KATIKA KANISA LA KKKT-RUAHA (MIKUMI)

Jana wakristo wote duniani kote waliungana ili kusheherekea sikukuu ya kukumbuka kufa na kufufuka kwa BWANA Yesu Kristo. Pasaka ni sikukuu ambayo hata kabla ya Yesu ilikuwepo na waisraeli waliisheherekea kama ishara ya kukumbuka ukombozi wa Jehova kuwatoa utumwani kwa kuwapigania ingawa kwa sasa dunia nzima tunaisheherekea kama ishara ya kumkumbuka BWANA Yesu aliyetukomboa katika utumwa wa dhambi. Kwa upande wa Mbunge mtarajiwa wa Morogoro katika Jimbo la Mikumi Joseph haule anaejulikana sana kama Profesa Jay alipata muariko kutoka katika Jumuiya ya wakristo kama mgeni rasmi. Muariko huu ni dalili nzuri kwake kwasababu inaonyesha ni jinsi gani hata viongozi wa dini wanamkubali na kumuheshimu kiasi cha kumpa nafasi muhimu kama hiyo ambayo wanasiasa wengi wanaitamani pasipo kuipata.
Kwa kuonyesha furaha aliyokuwa nayo Profesa Jay ambae pia ni mwanamuziki aliyeleta mapinduzi kwenye muziki wa Bongo Fleva na kuufanya uwe ajira kwa vijana wengi hapa Tanzania amepost katika page yake ya facebook kwamba "Namshukuru sana Mwenyezi Mungu pasaka yangu nimekula na wana Mikumi wenzangu Jimboni... Nilialikwa kuwa mgeni rasmi na jumuiya ya wakristo kwenye TAMASHA LA PASAKA pale Kkkt-Ruaha MUNGU NI MWEMA SANA!!"
Hongera sana Profesa Jay...

No comments:

Post a Comment