Sunday, April 5, 2015

LILIAN MARIKI MWANAMUZIKI WA NYIMBO ZA INJILI MWENYE CV INAYOVUTIA KUISOMA

Ukimtazama kwa haraka utasema ni Miss Tanzania au Model fulani wa kimataifa kwa jinsi anavyojiweka smart na jinsi anavyojua kupangilia pamba. Tofauti kabisa na wanamuziki wengi wa nyimbo za injili ambao wanajiweka shaghalabagala ili kuendana na tamaduni iliyozoeleka kwenye imani za kiroho hususani kwa wakristo wenye msimamo mkali na imani yao (Walokole). Liliani Mariki ameokoka na anampenda Yesu sana. Kuhusu huduma yake ya uimbaji alianza kuimba sunday school  tangia akiwa mdogo na akaendelea na huduma hiyo ya uimbaji hadi leo ambapo anaimba katika kikundi cha kusifu na kuabudu (Praise and Worship) kanisani kwao T.A.G.. God's Own International Church Skanska,  na Mchungaji wake ni Pastor Florence Lucas Mbago. Kwa upande wa kifamilia Lilian Mariki ni mke wa Mume mmoja na pia ni mama wa watoto wawili, Elimu yake ya juu ni mwanasheria ambae anamalizia masomo ya shahada ya sheria katika chuo fulani ambacho jina tuna lihifadhi. Mbali na huduma na elimu Lilian Mariki pia ni mjasiriamali anaemiliki duka lake lake la nguo pamoja na urembo wa wadada (boutique). Mungu amemuwezesha kurecord album yake ya kwanza mwaka juzi ambayo itakuwa tayari mwisho wa mwezi huu.
Katika huduma yake mwanadada Lilian amepitia changamoto na vikwazo vingi ambavyo yeye binafsi anaviona ni vya kawaida tu kwasababu safari yeyote ya kimafanikio haiwezi kukosa vikwazo "Wapo wanaonielewa na kunipokea vizuri lakini wapo baadhi ambao bado hawajanielewa na wananikosoa kwa kuwa kwenye jamii kuna itikadi mbalimbali za kiimani, lakini naamini itafika wakati watanielewa tu" Lisema Lilian. Kitu kikubwa kinachoweza kumsumbua ni pale anapokuwa amejiwekea malengo fulani ndani ya muda fulani alafu kutokana na majukumu mengine ya kifamilia akajikuta muda umepita na bado hajafanya jambo lolote. Lilian amesema kuwa japokuwa bado hajafika pale anapotaka kufika lakini kwa hatua hii aliyoifikia inamtia moyo na kuonyesha kuwa anachokifanya sio bure, japokuwa malengo yake ni kuliinua juu jina la Yesu duniani kote. Mwanamama smart Lilian Mariki amemalizia kwa kusema kwamba " Hivi karibuni natarajia kuachia video yangu  ambayo ina kiwango kizuri kuanzia audio mpaka picha"



No comments:

Post a Comment