Tuesday, April 7, 2015

MTUME PETER RASHIDI ABUBAKARI AFUNGUKA NA KUSEMA "MUNGU ANAPOAMUA KUMTUMIA MTU KATIKA VIWANGO VYA JUU HUWA HAANGALII WAPINZANI WANASEMAJE

Kuna usemi mmoja maarufu sana unaosema "when God say Yes no boddy can say no" usemi huu umechukua nafasi katika kauri aliyoitoa Mtume Peter Rashid wakati anazungumza na blog ya Makamanda.
Mtume Peter Rashid ambae anasimamia katika kanisa la Groly Of God lililopo mbezi mwisho karibu na kituo kipya cha mabasi. Mtume Peter Rashidi ambae zamani alikuwa ni muislamu lakini pia alikuwa anajishughulisha na kazi ya uganga wa kienyeji kabla ya kumjua Yesu, lakini baadae Yesu alimtokea na kumbadirisha kuwa mtumishi. Kabala ya kuanza kazi ya uhubiri Mtume Peter alipata mafunzo ya biblia toka katika vyuo vitatu vya biblia vilivyoko katika nchi tatu tofauti, " sijaanza huduma ya kichungaji au kitume nilisoma vyuo vitatu na vya nchi 3. Zambia(Ndola); Tanzania(Pefa-Kigoma); Kenya(Nairobi-East africa Bible College) ; Kila chuo nilisoma three years.  Alisema Mtume Peter Rashid. kwa njia ya simu.
Kuhusu swala la kushutumiwa kuoa mke wa pili na kumtelekeza mke wa kwanza amesema kwamba kwanza sio busara kumshutumu kwa jambo ambalo halijafanyiwa uchunguzi na wala hamlijui kiundani. "Nimegundua kuwa watu wanaweza kumshambulia mtu kwa kufuata mkumbo badala ya kufanya utafiti, na hata kama mtu amekengeuka huwezi kumsaidia kwa njia ya kumshambulia kwenye mitandao ya kijamii, bali unaweza kufanya kama jinsi Mungu alivyomtuma mtumishi wake Nathan kwa Mfalme Daudi pale alipomcchukua mke wa Ulia, Mm sikutaka kuoa mara baada ya yule mwanamke aliponikimbia na kuniita kafiri nilikaa kwa muda wa miaka sita (6) bila kuwa na wazo la kuoa. Ndio kupitia ushauri watumishi wa hapa Tanzania na nnje ya Tanzania waliponishauri ni heri nioe ili kuepuka tuhuma mbalimbali zinazoinuliwa na watu, ili utumishi wangu usilaumiwe. Ni afadhali sasa wananilaumu kwa kuwa nimeoa hilo naweza kustahimili ila nadhani ingekuwa ni aibu na ningepoteza ujasiri endapo ningekuwa nalaumiwa kwa ajili ya kubadirisha wanawake na wakati mimi ni mtumishi. Mtumishi wa Mungu Mtume Peter Rashid alimalizia kwa kusema "namshukuru Mungu anaenitetea kila iitwapo leo maana wengi wanajitahidi kunivunja moyo na kunikatisha tamaa kwa maneno yao lakini Mungu alivyo wa ajabu anazidi kunifariji na kunifungulia milango.
Mtume Peter Rashid Abubakar akiwa anafanya maombezi kwa baadhi ya waumini waliohudhulia ibada kanisani kwake

No comments:

Post a Comment