Monday, April 6, 2015

SIASA YA CCM KWENYE TAMASHA LA PASAKA IMESABABISHA MTUMISHI WA MUNGU MCHUNGAJI FAUSTINE MUNISHI ABANIWE KUIMBA KWENYE TAMASHA HILO

Katika mwaka wa kumi na tano (15) wa kusheherekea matamasha ya pasaka yanayoandaliwa na Msama Promotion, katika Tamasha lililofanyika jana imeonekana wazi siasa kuingilia kati. Kwenye tamasha hilo ambalo lina sifa ya kukusanya waimbaji mbalimbali wa kitanzania na wengine kutoka nnje ya Tanzania siku ya jana limezua mtafaruku mkubwa na kuwachanganya watu mbalimbali baada ya kuonekana mambo ni yaleyale ambayo yanajitokeza miaka yote. Watu wengi wamelalamika kuwa sound ilikuwa ni mbovu kama ilivyo kawaida ya maatamasha hayo miaka yote jambo ambalo wapenzi wa matamasha hayo wamekuwa wakiyalalamikia lakini hayatafutiwi ufumbuzi siku zote. Kwa upande wa waimbaji inasemekana wale wanaoitwa kutoka nnje ya nchi wanalipwa pesa nyingi sana tofauti na hawa waimbaj wa nyumbani ambao wao huwa wanajipeleka wenyewe kuomba nafasi za kuimba saa zingine hawalipwi hata shilingi kumi kwa madai kuwa wanajitangaza.
Tukiachila mbali hayo yote kubwa zaidi lililowakera watu wengi ni waandaaji wa Tamasha hilo kumuarika muimbaji mkongwe anaeheshimika sana Tanzania kwa ajili ya mchango wake mkubwa wa kuihubiri injili kwa njia ya nyimbo Mchungaji Faustine Munishi kunyimwa nafasi ya kupanda stejini licha ya kuarikwa na kutangazwa redioni. Watu wengi sana walihudhuria tamasha hilo baada ya kujua kuwa Munushi yupo na wakati uimbaji unaendelea kundi la watu lilionyesha kumtaja mumbaj huyo kuwa wanamtaka apande stejini kuimba lakini ikawa ni ngumu na waandaaji hawakumpandisha hadi tamasha lilipokwisha.
Hakuna asiyejua tofauti iliyopo kati ya Mchungaji huyo na chama cha mapinduzi, na kwa sababu Mgeni rasmi alikuwa ni Waziri wa Mambo ya nnje Muheshimiwa Benard Membe hali hiyo imetafsirika kuwa huenda Mchungaji Fustine Munishi amenyimwa nafasi hiyo kwa sababu Membe angemuona inawezekana mahusiano kati ya Msama na CCM yangepungua ndio maana wakamtoa kafara na kumuacha akiwa uwanjani back stage amekaa anangojea kuimba hadi mida ya saa tatu tamasha lilipoisha na hakupewa nafasi kabisa. Siasa kuingia hadi kwenye matamasha ya injili hii n hatari sana kwa kanisa..

No comments:

Post a Comment