Siku chache baada ya
kuzinduliwa kwa treni mpya ya abiria (Deluxe), abiria wa awali kutumia
usafiri huo kutoka Dar es Salaam kwenda Kigoma, wamekosa ustaarabu na
kufanya uharibifu katika baadhi ya mabehewa. Akizungumza mjini Kigoma,
Meneja wa treni hiyo, Jonas Afumwisye, alisema baada ya kufika Kigoma,
waliifanyia ukaguzi, ndipo wakagundua kuwepo kwa uharibifu katika baadhi
ya vyumba vya daraja la pili na sehemu ya daraja la tatu la treni h
iyo.
Alitaja moja ya maeneo yaliyoharibiwa kuwa ni pamoja na kung’olewa kwa
mkono wa kupandishia na kushusha kitanda cha kati katika chumba cha
daraja la pili. Mbali na kung’oa kabisa mkono huo wa kitanda, kwenye
moja ya mabehewa ya daraja la tatu, abiria wameng’oa baadhi ya mapazia
hatua iliyosikitisha uongozi wa Kampuni ya Reli (TRL), ambao umekusudia
safari za treni hiyo ziongezeke kutoka mbili hadi tatu kwa wiki tofauti
na ile ya zamani.
No comments:
Post a Comment