Friday, April 3, 2015

Msala uliompata Mchungaji Gwajima wa kumtolea maneno yenye kuudhi Askofu wa Kanisa Katoliki Mwadhama Polycap Kadinali Pendo na kisha kuhojiwa polisi na kupata mshtuko, kuzimia hadi kulazwa, Mume wa Flora Mbasha, anasema hayo ni malipo ya Mungu kwake kutokana na kilio chake baada ya Mchungaji huyo kusambaratisha ndoa yake .
“Ile hali ya Gwajima ni malipo. Mimi nilishasema jamani, mtu akikutendea ubaya malipo ni hapahapa duniani, hakuna kwingine. Mimi ndoa yangu haipo, mke wangu anajua yeye anavyoishi. Kwa hivyo mimi nimekuwa nikiishi kwa manung’uniko kila siku, unadhani nini kitatokea kwake?” amefunguka Emmanuel Mbasha
Chanzo cha habari hizi ni page ya East Africa Television...

No comments:

Post a Comment