Friday, April 10, 2015

NABII MKUU DR GEOR DAVIE ATABIRI KUHUSU MAJANGA MBALIMBALI YANAYOTOKEA NCHINI TANZANIA

Balozi wa Nabii Mkuu Dr Geor Davie amewataka viongozi wa Tanzania wasikilize maonyo na nabii zinazotolewa na Nabii Geor Davie. Balozi huyo anaejulikana kwa jina la Apostle Sekela ameyasema hayo kupitia ukurasa wake wa facebook ambapo ameandika kama ninavyo nukuu "Watanzania na viongozi wa Taifa hili tujue na tuelewe kuwa Mungu anatupenda kwani katuinulia Nabii Mkuu ktk nchi yetu basi tumsikie yeye.
Siku chache zilizopita Nabii Mkuu Dr GeorDavie alisema kuhusu hali ya nchi.alisema kuanzia hapo mpaka mwezi wa sita kutakuwa na majanga na kuna mambo yatasikika.Toka alipoongea tu kesho yake tukasikia yale yaliyotokea kule Amboni Tanga.
Na sasa tunasikia tetesi ya majanga hasa haya mambo ya magaidi.
Ni kweli watu wanaomba kwa Mungu ili tuepushwe na hayo ila turudi kwenye msingi wa Neno la Mungu.
2 Nyakati 20 Sura hii inatuonyesha jinsi ambavyo mfalme Yehoshafati alivyoambiwa juu ya maadui walivyojipanga kuvamia nchi yao.
Tunasoma jinsi walimtafuta Bwana na kuomba na Mungu aliwajibu kwa kumtuma Nabii ambaye aliwapa maagizo kitu cha kufanya.
Mstari wa 20 Mfalme aliwaambia watu .....; Waaminini manabii wake ndivyo mtakavyofanikiwa.
Biblia inasema hayo yote ni kivuli cha mambo haya tuliyonayo sasa sisi ndio tuko kwenye picha kamili.
Kama wao walifanikiwa kwa kumwamini Nabii kwetu leo ni zaidi.
Tena sisi tuko ktk wakati ulio bora kwani Mungu katuonyesha mapema yatakayokuja kupitia Nabii wake na alitupa njia ya kupona ktk hayo.
Nabii mkuu Dr GeorDavie alisema tutoe sadaka ya kuepushwa na majanga.
Unaweza kufanya hivyo kama unamwamini Nabii.na kama viongozi wangetii nchi yetu ingepona kabisa."

Mwisho wa kunukuu..
 

No comments:

Post a Comment