Kutokana na wimbi kubwa la imani kuibuka katika nyakati hizi za karne 21 huku watumishi wengi wakionekana kuzama na kuibuka na maufunuo na mandotondoto na mavocal maziitoooo ya kuwatishia watu ili kuwaweka chini ya milki yao kama vijakazi badala ya kuwafundisha kweli ya Kristo itakayowaweka huru, Mtumishi wa Mungu Nickodemus Shaboka ameamua kuinuka na kuvunja ukimya.
Mtumishi huyo ambae ni mume halali wa Rose Mushi yule mchumi na mwalimu pia muandaaji wa makongamano ya wanawake yanayojulikana kama Ladies Of Destiny, ambae baada ya kuolewa amebadilisha jina na kufuata ubini wa mume wake na kwasasa anajulikana kama Rose Shaboka, ameamua kusimama na kuzungumza kweli kuhusiana na neno la Mungu. Mtumishi wa Mungu Nickodemus ameorodhesha tabia na dalili zote za watumishi walioanza vizuri na baadae wakajikuta wamekengeuka na kuiacha njia ya BWANA huku wakizifuata tamaa za wenyewe. Na hili ndilo somo aliloliandika kwenye ukurasa wake wa facebook ambalo limeonekana kupokelewa vizuri na mamia ya watu.. Nanukuu " TAHADHARI.
Ukiona Mchungaji, Mtume, Nabii au kiongozi wako wa
kiroho anaanza kujipa nafasi ya Mungu na kukuhubiria kuwa ukimkosea yeye
anaweza kukufungia usimuone Mungu wala usiingie mbinguni, hilo kanisa
hama mara moja. Unapoona kiongozi wa kiroho anaanza kujiinua yeye kuliko
Kristo Yesu fahamu ameshaiacha njia. (Yohana 12:32), Yesu pekee ndio
njia ya kukufikisha kwa Mungu. Hakuna nabii yeyote ambaye kwa kumwamini
yeye unapata uzima wa milele isipokuwa kwa kumwamini Yesu. (Yohana 14:6) Tafuta mahali Kristo anahubiriwa ukalelewe kiroho.
Pazia la hekalu limepasuka kutoka chini mpaka juu hata watu wa ua wa
nje walipata access ya kuona patakati pa patakatifu (Marko 15:38).
Asikutishe mtu ati yeye yuko karibu na Mungu kuliko wengine. Hata wewe
unaweza kuwa karibu na Mungu ukiamua.(Yakobo 4:8) Kwani ukimtafuta
anapatikana. (Yeremia 29:13 ) Yesu alikuja ili kila amwaminiye yeye
(Yesu) asipotee bali awe na uzima wa milele. (Yohana 3:16, Warumi
10:9-10). Yesu ndio kila kitu, yeye habadiliki (Hebrania 13:8) wengine
wote wanaweza kubadilika. Weka tumaini kwa Yesu utakuwa salama. Sisemi
usiheshimu wachungaji,mitume na manabii wanaokuongoza, hapana ila
chunguza, je wanamuhubiri Kristo au wanajihubiri wao? Ukiona injili zao
zimejaa kujifagilia wao wenyewe na hakuna Yesu, hapo kimbia kabla
hujachomwa moto. (Galatia 1:6-10) Yeyote ambaye anahubiri injili
nyingine mbali na hii ya kuwa Yesu ndio njia pekee ya uzima wa milele.
Yesu ndio mwanakondoo wa Mungu aondoaye dhambi za ulimwengu. (Yohana
1:29)Yesu ndio mjumbe wa agano jipya(Waebrania 12:24). Yesu ndio ufufuo
na uzima(Yohana 11:25) ni damu ya Yesu pekee yenye kuondoa dhambi
(Mathayo 26:28)
YEYOTE ANAYEHUBIRI TOFAUTI NA HAYO NA ALAANIWE NA WATU WOTE WASEME AMINA."
No comments:
Post a Comment