Hii ni ndani ya mkesha wa Mega Church 2015 uliofanyikia ubungo extenal ktika kanisa la Victorious Church linaloongozwa na mchungaji John Saidi. Kwa kweli mkesha ulikuwa bomba sana wa kimataifa ambao ulikusanya watu wengi sana. Miongoni mwa waimbaji walioimba kwenye mkesha huo ni pamoja na Kuhani Zangina aliyejulikana kama Mtoto wa Mchungaji enzi hizo, ambae alihudumu kwa kuimba wimbo wake wa Vunja Ngome za Shetani, Pamoja na Apostle Bashando aliyeimba wimbo wa Nyeyekea, baada ya hapo kulikuwa na shuhuda, na baada ya shuhuda yalifuatia maombi mazito ya kuliombea taifa katika wakati huu tunapouelekea uchaguzi mkuu. Mkesha mwingine utafanyika tarehe 1/May/2015 ambao utaambatana na sherehe ya kutimiza miaka kadhaa ya jengo la kanisa hilo. Hakikisha haukosi mkesha ujao maana itakuwa ni fireeeeee 4 fireeeeee
No comments:
Post a Comment