Wednesday, April 8, 2015

TAZAMA PICHA ZA MPEMBA WA KWANZA KUOKOKA AKIWA NA MASTAR MBALIMBALI KATIKA TASNIA YA INJILI

Mpemba wa kwanza kuokoka akiwa na Muimbaji John Lisu

Mpemba wa kwanza kuokoka akiwa na Mbasha .

Mpemba wa kwanza kuokoka akiigiza kupokea tuzo toka kwa (George Mpela )

Mpemba wa kwanza kuokoka ni mwanamuziki wa nyimbo za injili mwenye juhudi katika kazi ya BWANA na pia ni muandaaji wa matamasha mbalimbali. Mara ya kwanza nilikutana nae katika tamasha la uzinduzi wa album ya Angel Benard.
Ni kijana mmoja mchangamfu na muongeaji sana, mara nyingi tumekuwa tukichat mitandaoni tu, lakini mara ya pili kuonana ilikuwa ni Arusha ambapo alikuwa ameenda kushoot video ya album yake.

Ni miongoni mwa vijana wenye vision kubwa sana katika mziki wa injili, na moja kati ya ndoto alizo nazo ni kuja kuwa promota mkubwa kama yule jamaa anaeandaa haya matamasha ya injili.

Kwa mitandaoni Jina lake analotambulika nalo ni Abuu Levy, na lingine anafahamika kama Mpemba wa kwanza wa kuokoka.

Kwa sasa anafanya kazi na kiango media lakini pia ana huduma yake inayoitwa Mwarabu Ministry, sijui kama imesajiliwa lakini ipo.
Mungu ambariki na kumuinua huyu kijana..
Na mwandishi wetu

Mpemba wa kwanza kuokoka akijiandaa kupiga picha na Emmanuel Mbasha


No comments:

Post a Comment