Alianza kujulikana mwanzoni mwa miaka ya 2000 baada ya kutoa single ya R&B inayoitwa "Machozi" tangia hapo aliendelea kufanya vizuri kimuziki, mwanadada wa kikurya Judith Wambura maarufu kama Lady JayDee ambae anatokea katika familia ya kisabato na inasemekana alikuwa ni mwanakwaya mzuri tu kanisani hapo, sasa ameanza kufanya madudu. Mara kwa mara wanamuziki wenzake wamekuwa wamsifia sana kwa uwezo wake wa kujimanage na kujua namna ya kujishughulisha kwa ujasiriamali huku akipata sifa kadha wa kadha, hivi sasa Lady JayDee anaonekana kupoteza muelekeo na kuanza kupunguza mvuto kutokana na mambo ya ajabu anayoyafanya. Mwanadada huyo ambae hayuko kwenye mahusiano mazuri na mumewe walioishi zaidi ya miaka kumi, mara kadhaa amesikika akimponda mumewe radioni, jambo ambalo watu wengi wamekuwa wakikereka nalo. Mbaya zaidi sasa hata ameanza kuwavunja moyo watu wasiohusudu mambo ya kishirikina kwa jinsi anavyoyapa kipaumbele. Wiki iliyopita Lady JayDee alimualika Mtabiri na msoma nyota katika kipindi chake cha (DIARY YA
LADY JAYDEE) ili amtabirie, yule msoma nyota akamtabiria Lady JayDee kupata fedha nyingi sana mwaka huu
2015 kupitia muziki wake lakini kwa upande wa afya yake ataumwa kidogo
na kufikiria kifo mara kwa mara lakini hatokufa. Pia akamtabiria Jay Dee
kuolewa na mwanaume tajiri na maarufu 2015/2016. Jambo hilo limewakera baadhi ya mashabiki wake ambao katika imani zao hawaamini kusomewa nyota wala kutabiriwa na wapiga ramri. Na kumuona kama ameanza kupotosha jamii kwa kupromote imani ambazo hazifai.
No comments:
Post a Comment