Monday, April 13, 2015

YALIYOJIRI ZANZIBAR, KIJANA AKUTWA AMEJINYONGA KATIKA HOTELI ALIYOKUWA AMEKODISHA CHUMBA

 Kijana mmoja wa asili ya kiarabu alitoka Oman akakodi chumba hoteli moja Zanzibar, akawa analewa tuu, sasa pale hoteli wakamuomba pesa za chumba akawaambia angewapa asubuhi ya jana. Wahudumu hiyo jana asubuhi wakaenda kumgongea ili alipe pesa ya chumba, baada ya kugonga kwa muda mrefu wakaona hafungui ndipo walipoamua kuvunja mlango na wakashangaa kukuta jamaa kaisha jinyonga kitambo.

No comments:

Post a Comment