MWANAHARAKATI DOUGLAS PIUS (DP) MTANGAZAJI WA RADIO ALIYETOKEA KWENYE MUZIKI WA INJILI
Ni mume wa mke mmoja na baba wa watoto wawili ambae ameyatoa maisha yake yote katika kutimza ndoto zake. Dp ni kijana anaejiamini sana na pia anaamini kuwa kila anachokihitaji kinaweza kupatikana haijalishi kina gharama kiasi gani. Alianza na kuimba nyimbo za bongo fleva enzi hizo miaka ya 2000 hadi 2003 alipohamia kwenye mziki wa injili. Alikuwa na kundimoja lililojiita kundi la swahili, na walifanikiwa kutoa single mbili ambazo zilihit hapa bongo, wakati anaendelea na safari yake ya bongo fleva Mungu alimuita njiani ili aje kumtumikia katika nyimbo za injili. Akahamia huku kwenye uwanja wa Yesu ambapo aliimba injili lakini kwa muendelezo wa mahadhi yaleyale ya bongo fleva, jambolililomuwia ugumu kiasi kwakuwa wapendwa walikuwa hawaelewi kabisa mtindo huo na kuhesabu kama ni uhuni unaoingizwa kanisani kwa siri. Pamoja na yote hayo lakini hakukata tamaa kwa sababu ndoto zake hazikumtuma kufanya jambo lolote tofauti na hicho anachokifanya. Mnamo miaka ya 2005 alikutana na George Mpela ambae n Mtangazaji wa Praise power radio na wakaungana pamoja na waimbaji wengine kama vile Rungu la Yesu, Baltazaar Paul, Henry Potea, na wengine wengi ambao asilimia kubwa walikuwa wanaimba nyimbo za mahadhi ya kiujana zaidi na wakaanzisha umoja wao na kujiita Youth Gospel Family, kwakweli kwa zama hizo walifanya vizuri hasa katika kuandaa matamasha na kuutambulisha muziki wa kizazi kipya wenye ujumbe wa injili ndani yake.
Baada ya muda kundi hilo la Youth Gospel lilisambaratika baada ya tofauti kuanza kutokea huku baadhi ya wana youth wakionyesha ubinafsi na huku wakijiona wao ni maarufu zaidi ya members wengine ndani ya kundi hilo na kuanza kujitenga. Wakati hayo yote yanaendelea Dp alikuwa yuko Chuo anasomea biblia (Bible school). Baada ya kumaliza chuo alihamia katika mkoa wa Mbeya na huko ndio alipoanzia kutangaza katika radio. Amefanya kazi kwa zaidi ya miaka mitatu huko mbeya na kwasababu ana juhudi katika kile anachokifanya sifa zake zilivuma hadi zikafika katika radio ya hapa dar es salaam, akapigiwa simu na kuitwa, na alipokuja akaanza kufanya kazi katika kituo cha Praise Power Radio ambapo hapo ndio alitumia nguvu zote kuutambulisha mziki wa Gospel Hip Hop ambao ulikuwa hauheshimiwi na unadharaulika sana. Wakati anaendelea na kazi alipata tena wazo la kuanzisha kundi lingine ambalo litaweza kufanya vizuri katika medani ya muziki wa injili na kuleta mabadiriko makubwa, ndipo Dp akamuita rafiki yake Henry Potea pamoja na Bashando na kuwashirikisha wazo lake na muafaka wao ikawa ni kuanzisha kundi litakalojulikana kwa jina la Gospel Revival Generation (GRG).
Kundi hilililianza kufanya kazi zake vizuri mnamo mwaka 2010 kwa kuandaa matamasha makubwa ambayo yaliwakutanisha watumishi na waimbaji mbalimbali, vilevile likautambulisha muziki wa kizazi kipya katika mahadhi ya injli vizuri sana, Hatimaye wana Hip Hop ambao walikuwa wanabaniwa kupigiwa nyimbo zao kwenye radio wakaanza kupata air time ya kutosha, na angarau majina yao yakaanza kutambulika, lakini kwasababu katika wingi hapakosekani unafiki bado kuna wengine wachache walianza kujitenga polepole na kuanzisha makundi pembeni huku wakizibeza juhudi za Dp, ingawa ilimuumiza moyo lakini hakukata tamaa kwasababu anaamini katika ndoto hapakosekani na upinzani.
Wakati yote hayo yanaendelea Dp alikuwa yuko chuo anasomea Diploma ya uandishi wa habari na wakati huohuo akawa ameanzisha kundi lingine la Unity Family ambalo kwa malengo ya kuweka ushirikiano kati ya wana Unity na GRG katika kuzisukuma harakati. Mwaka 2013 Dp alihama kikazi kutoka Praise Power Radio na kwenda Clouds Fm Radio ya Watu akiwa kama producer ambapo hadi leo yuko hapo. Na anaendeleza harakati zake, kupitia movement zake amewatambulisha waimbaji wengi wa Gospel Hip Hop na Wa mahadhi ya kawaida na ndoto zake ni kuikamata Afrika.
No comments:
Post a Comment