NABII HONEST MALLYA NA MUIGIZAJI WA FILAM MNIGERIA RAMSEY NI KAMA MAPACHA
Katika ukurasa wake wa facebook Nabii Honest Mallya amepost picha iliyoeditiwa na kuonyesha kuwa yuko karibu na Ramsey, huku akiwa ameandika maneo haya "Pokea amani kati yako na mume wako na mke wako kwa jina la Yesu". Picha hiyo mbayo imeonyesha kuwashtua na kuwapa maswali baadhi ya watu wanaomfuatilia imebidi wengine wafunguke na kuanza kuhoji kama Ramsey nae ni mtumishi wa Mungu? Lakini Nabii Mallya akajibu kuwa Ramsey ni rafiki yake.
Nabii Mallya ambae Mungu anamtumia kwa viwango vikubwa sana, ijumaa iliyopita aliuwasha moto wa katika mkesha uliofanyika kanisani kwa Apostle Pke PatrickKayimbi Emmanuel na watu wakafunguliwakupita maelezo.
Ukimuona ni mtumishi smart sana na pia mambo yake huwa anayazungumza katika njia ya kawaida kabisa lakini baada ya muda ni lazima yatatokea. Kwa mfano miezi michache iliyopita amewahi kutoa unabii wakati akiwa anahubiri kwenye kongamano moja kanisani kwa Apostle Komanya kwamba "Kuna ndege itaanguka lakini watu waliomo ndani yake watapona, na kweli kesho yake ilitokea kama alivyotabiri na yule rubani aliyepona alikwenda kumuona Nabii Mallya kanisani kwake.
Hivi karibuni tu Nabii Mallya ametoa unabii kwamba kama waganga wa kienyeji wasipotubu na kuacha uganga wao Mungu anakwenda kuwaua, na kiongozi yeyote atakaeenda kwa waganga kutafuta nafasi ya uongozi hata akupata hataweza kukaa kwa zaidi ya miezi mitatu katika kiti hicho pasipo kukiacha kwa kufa ghafla. Japokuwa unabii huu ulipata changamoto sana haswa kwa kundi la waasi lililojitokeza na kupingana nae lakini Nabii Mallya alisema yeye haongei sana ila watu wasubilie tu wakati wa unabii huo kutimia kwasababu anamjua Mungu aliyemtuma.
No comments:
Post a Comment