Wednesday, April 8, 2015

MTUME IBRAHIM PETER NA MKE WAKE WAUWASHA MOTO DODOMA, NI KATIKA SEMINA YA PASAKA AMBAYO ILIMTEKETEZA SHETANI NA VIWAKALA VYAKE

Mtumishi wa Mungu Abraham Peter, amekuwa na ziara ya kitume ya pasaka mjini Dodoma. Katika ziara hiyo amefanya semina katika eneo la kisasa ndani ya kanisa la Naini Miracle International linalochungwa na Nabii Petro Kagayambe. Semina hiyo ilihusu pasaka ya kwanza ya waisrael toka utumwani siku ambayo Mungu aliachilia pigo la mwisho kwa wamisri, Katika semina hiyo ambayo Mtumishi wa Mungu Abraham Peter aliambatana na mke wake, siku moja Mama mtumishi ndio alisimama madhabahuni na kuanza kuwasha fireeeeeeeeeeeeeeeeeeee hakika watu waliponywa,kufunguliwa toka katika vifungo vyao, na hakika ilikuwa baraka tele wakazi wa Dodoma.
Mtume Abraham Peter akiendelea na mahubiri ya ukombozi

Waumini wakifuatilia mafundisho ya mtume Abraham Peter
 
Mtume Abraham Peter akimfungua kijana toka katika kifungo cha shetani

No comments:

Post a Comment