Kutokana na sakata la pengo na Gwajima kila mtu anajua kinachoendelea, polisi walimuita Askofu Gwajima kwa ajili ya mahojiano na Askofu akazimia akiwa polisi na kupelekwa TMJ hospital, lakini baada ya siku mbili Kadinali Pengo alitamka hadharani kuwa amemsamehe na wala hana neno nae. Jambo la kushangaza sana aliyepaswa kulalamika ameshasamehe, na wala sio yeye aliyefungua kesi, bali aliyefungua kesi ni jamaa mmoja fundi Selemara ambae hata sio mkatoliki bali ni muislamu, na kinachoendelea kushangaza watu Jana Askofu Gwajima kaitwa tena polisi, na alipofika kwenye mahojiano dhidi ya kesi inayomkabiri ya kutoa lugha chafu za kashfa dhidi ya Kiongozi mwenzake wa dini Kadnali Pengo, wao wametaka ajielezee mali alizokuwa nazo, Helkoptel anayomiliki, miradi aliyo nayo pamoja na kuwaorodhesha ndugu zake wote walio hai na waliokufa jambo ambalo halihusiani kabisa na kesi aliyofunguliwa. Swala hili limenipa maswali mengi sana juu ya kesi hii na kunifanya nibakie najiuliza je, hii ni kesi ina mkono wa nani nyuma yake? Maana hapa inaonyesha kama kuna namna fulani jeshi la polisi linaweza kuwa linatumika kisiasa jambo ambalo si halali kwa jeshi hilo. Miezi michache iliyopita Askofu Gwajima alimuonya C.A.G kwa kitendo chake chakutumia pesa za uma kujengea msikiti jambo ambalo lilimfanya apanic nakuanza kumshambulia Gwajima kwenye mtandao wa kijamii kupitia ukurasa wake wa facebook, sasa sijui kama yaliisha ila nahofia sana hadi yale yasije kuwa yamejumuishwa humu ili kuzidi kumkandamiza Bishop Gwajima pamoja na kumziba mdomo pale anapoona mambo maovu yanayofanyika chinichini na kuyalipua hadharani.
No comments:
Post a Comment