Mtumishi wa Mungu Edwin Seleli aka Big Daddy E amejikuta akikaribia kupita kwenye dirisha la gari baada ya polisi kuanza kufyatua mabomu ya machozi ubungo. Mtumishi huyu ambae alikuwa ana safari ya kwenda Geita alifika Ubungo mapema sana leo hii ili kuwahi usafiri, pasipo kujua leo ni siku ambayo madereva wamegoma. Akiwa kituoni hapo na hajui hatma ya safari yake ilimbidi aendelee kukaa ndani ya gari ili kupata muafaka, akiwa ndani ya basi kwa takribani masaa mawili mara ghafla alisikia sauti kubwa ya kishindo cha bomu, wakati ametaharuki na kudhania huenda ni alshababu wamevamia hapo alishangaa hali ya hewa ikibadirika na kumsababisha aanze kukohoa huku machozi yanamtoka pasipo yeye mwenyewe kutaka. Alipokuwa akiongea na blog ya makamanda Edwin Seleli alisema "Nilikua ndani ya bus, yalipotandikwa mabomu,
weeee, dirisha nililiona ni kubwa kama geti ningetosha kabisa hayaa
mambo muhadithiwe tu si kuyaona na kusikia ile mambo ikipasuka kwanza
mlio kisha unaanza kulia bila kupenda na kukohoa- sijui wanaweka
pilipili kichaaaa dah"
Pole sana kamanda wangu ndio hali ya nchi yetu hiyo........
Ahahahahahha pole sana our friend Edwin Seleli this is Tz, just soon you will get used. So, you are warmly welcome.
ReplyDelete