Friday, April 10, 2015

KUTANA NA MWANAKWAYA ALIYEGEUKIA KWENYE BIASHARA YA BIA, HIVI SASA ANAMILIKI BAR SINZA NA ANAKUNYWA ILE MBAYA

Dada mmoja  aliyekuwa anaimba kwaya ya bugando iliyokuwa ikizunguka na Mzee Kulola enzi za uhai wake inasemekana amemuasi BWANA na kuanza kujishughulisha na shuguli za kuuza pombe. Dada huyu aliyekuwa ameokoka kabisa na amekulia kwa late Bishop Kulora EAGT. Huko mwanza wazazi wake walikosa uwezo wa kumsomesha hivyo akasomeshwa na Askofu kulora mpaka akapata Diploma ya Accounting chuo cha CBE Mwanza, alikuwa ni muumini mzuri sana na mwimba kwaya ya Bugando iliyokuwa ikizunguka na Askofu Kulora ktk enzi za huduma yake. Chanzo cha habari kinasema binti huyu alikataa wachumba kama zaidi ya wanne walio okoka kisha akaja kuolewa na mtu ambae hajaokoka lakini yuko vizuri kiuchumi, "yaani tangu aolewe haendi tena kanisani bali kazi yake ni kushinda kwenye bar ya mume wake huku anakunywa na kuuza bia.'' kilisema chanzo hicho.. Blog ya makamanda tuko kwenye maombi kumuombea dada yetu ili aweze kumrudia Mungu maana tunajua hilo ni jaribu ambalo mkono wa BWANA unaweza kumchomoa huko....

3 comments: