Huyu ni mcheza miereka mwenye juhudi na asiyekata tamaa kiasi kwamba ukifuatilia mapambano yake utajikuta unaanza kuupenda huu mchezo wa miereka. Sifa kubwa ya John Cena ni kupenda haki bila kutumia njia za mkato ili kufikia mafanikio yake. Katika medani ya mchezo huo anajulikana sana kama kwa slogan yake nayosema Hustle, Royality and Respect.
John Cena baada ya kushinda mkanda wa United State Championship |
John Cena amewahi kushikiria mkanda wa dunia baada ya kumshinda The Big Show, na baadae akaja kuushikilia mkanda wa WWE na kudumu nao kwa takriban miaka miwili. John Cena mcheza miereka anaeongoza kwa kupendwa na watu alianza kushuka kiwango baada ya kushindwa na Shymus zaidi ya mara mbili, na baadae alipunguza idadi ya mashabiki wake baada ya kupangiwa mechi na The Rock, jamaa ambae ndio kinara wa mchezo huo. Inasemekana hata kilichomtoa John Cena ni pamoja na kuiga baadhi ya style za The Rock ambae kwa sasa yuko Hollwood anaigiza movie.
John Cena ambae kwa muda mrefu sana alikaa bila mkanda wa aina yeyote jambo ambalo lilikuwa linamuumiza moyo hatimaye kwenye mechi ya Wrestlemania 31 iliyochezwa tarehe 28/March/2015 alipigana na Mrusi anaejulikana kwa jina la Rusev ambae ndio aliyekuwa anaushikilia mkanda wa United State Championship, Huyu mrusi ni mpiganaji hatari ambae hana historia ya kushindwa, na katika record yake ameshawashinda wacheza miereka matata sana kama vile Mark Henry, The Big Show, Jack Swager pamoja na wengine wengi. Rusev ni Mrusi asiyelipenda kabisa taifa la Marekani na kila anaposimama haachi kulitukana jambolililomfanya John Cena aahidi kumziba kinywa chake. Ingawa katika pambano la kwanza alifanikiwa kumshinda Cenna tena kwa knock out lakini sina bado aliomba re-match ambapo katika siku ya jumapili ya tar 28 ndio walipigana.
No comments:
Post a Comment