Wednesday, April 1, 2015

YOU NEED STRONG SPIRITUAL RANKS TO BATTLE WITCHCRAFT
Kuna nguvu nyingi za kichawi katika ulimwengu tunaoishi, sawa sawa na neno la Mungu katika kitabu cha Ufunuo 2:13 Napajua ukaapo, ndipo penye kiti cha enzi cha Shetani.....Kuna uchawi mwingi kwenye jamii tunazo ishi, kwenye biashara, kwenye siasa nk. Ili uweze ku-rule kwenye ulimwengu uliojaa nguvu za kichawi Unahitaji Ranks. Kwenye ulimwengu wa biashara kuna uchawi, kwenye ulimwengu wa siasa kuna uovu na uchawi, Wewe lazima upande Ranks ili uweze kushinda, sio tu kuwa Mkristo hiyo haitoshi. 1 Korintho14:32, Hesabu 22:15, 1falme 18:40.
Ili uweze kushinda, unahitaji kumpokea Yesu. Unapompokea Yesu unaganyika kuwa Mwana wa Mungu. Yohana 1:12, Zaburi 89:27.
Tunapompokea Yesu tunapewa Rank ya Kufanyika Wana..Baada ya kumpokea Yesu Unafundishwa na unapopata funuo na mafundisho yanakukuza kutoka kwenye uwana na kuwa matured ambapo unaongezeka rank.Ebrania 5;10 -14, Galatia 4:3.
Ukristo ni kupanda Rank siku hadi siku, si kudumaa na kubaki hivyo hivyo toka ulipobatizwa.
Rank hushinda Rank nyingine. Lazima tupande Rank ili tuweze kushinda uovu na nguvu za kichawi.
Witchcraft imekuwa na nguvu kwasababu Wakristo hawapandi Rank.
Kuwa na kiu ya kupanda Rank ili uweze kushinda.

No comments:

Post a Comment