Muimbaji wa Nyimbo za injili kamanda Joseph Nyuki ameamua kutupilia mbali ubrother men na mashauzi ya kistar ambayo waimbaji wengi wamekuwa wakiyaonyesha na kuamua kuipiga kazi ya BWANA kikamanda kama mitume tunavyofanya. Nyuki ni muimbaji mwenye mkono mmoja ambae alianzia na kucheza show kwenye maharusi mbalimbali na katika kumbi za starehe, lakini baadae aliokoka na kuanza kuimba na kucheza kwa lengo la kumtukuza Mungu. Kipaji chake na juhudi zake zimekuwa ndio sababu kubwa sana ya kumpatia miariko mingi toka sehemu mbalimbali achilia ile hali inayomtambulisha ya kutokuwa na mkono mmoja. Kwakweli huyu kamanda amejijengea jina sana katika muziki wa injili Tanzania, na hadhi yake ni kubwa kihuduma kiasi kwamba maisha aliyopaswa kuishi ni yale maisha ya anasa ambayo waimbaji wengi wa injili wamejipangia na kuyapa kipaumbele.
Miaka ya hivi karibuni Kamanda Joseph Nyuki alienda Nirobi hukoKenya kwa ajili ya shughuli za kimuziki, lakini baada ya kutoka huko alikuja na staili mpya ambayo waimbaji wengi wameiita kama ni aina fulani ya kujidharirisha, lakini kwa bahatinzuri nilipokutana na Nyuki mkoani Arusha alinielezea nia na madhumuni ya yeye kufanya hivyo. Siku hizi Nyuki sio muimbaji wa kujifungia chumbanina kungojea miariko ya huduma ambayo atalipwa shilingi milioni moja itakayoambatana na maneno ya shutuma kama ilivyo kwa waimbaji wengi, na isitoshe ile dhambi ya kutoa rushwa redioni ili nyimbo zake zipigwe ajulikane na kuitwa katika makanisa na mikutano ya injili au harusi amekwisha ondokana nayo kwasababu ameamua kufanya uinjilisti wa barabarani. Anakuwa anatembea na gari ndogo zile canter aina ya Kirikuu, ambayo inakuwa imefungwa mziki mzito
ambao kila wakati wanapiga nyimbo zake huku yeye akiwa anaimba barabarani na kucheza. Na watu wakikusanyika anawauzia cd zake huku hapo hapo anawahubiria habari njema za Yesu Kristo. Kupitia huduma hii ambayo wengi wameihesabu kama ni njia ya upuuzi na kujidharirisha, lakini kwa Joseph Nyuki hali ni tofauti kabisa, maana kwake ni kazi inayomuingizia kipato kwa njia ya kuuza cd, pili ni huduma inayowaleta watu wengi kwa Yesu. Malengo ya Joseph Nyuki ni kununua gari ya aina ya Vorg ndani ya mwaka huu...
No comments:
Post a Comment