Wapenzi wasomaji wa blog ya Makamanda naomba nichukue nafasi hii kuzungumza na mdogo wangu Rich Mavoko ambae ni muimbaji wa Bongo fleva, lengo langu sio kumponda bali nikumuweka sawa kama kaka ambae kwa maswala mengi nina upeo mkubwa sana zaidi yake. Mimi ni miongoni mwa watumishi wachache ambao sina tatizo na kusikiliza muziki wa aina yeyote, hivyo katika flash yangu nina baadhi ya nyimbo za bongo fleva ambazo huwa nazisikiliza, na kweli kabisa nazungumza, katika bongo fleva kuna wasanii ambao nawafuatilia sana na ninapenda kazi zao ingawa zina mapungufu, lakini huwa nikiwasikiliza naona kabisa wana nafasi ya kufanya vizuri na kuijenga jamii yetu endapo wakipata ushauri toka kwa watu makini kama mimi. Miongo mwa wasanii hao ni Christian Bella, Diamond Plutnum, Rich Mavoko, Rama Dee, na Profesor Jay. Kwakweli hawa watu nawakubali na ninawaombea kwa Mungu injili ipenye ndani yao. Ila katika kuwapenda na kuyaona mapungufu yao, naomba nitumie ukurasa huu ama blog hii kuwakosoa kila ninapopata nafasi. Leo nitaanza na Rich Mavoko na hawa wengine watafuatia siku nyingine. Huyu kijana Rich Mavoko ana wimbo wake mmoja unaitwa roho yangu, na katika verse ya wimbo huo kuna neno kalitumia linalosema "HAYA MANENO WALISEMA WAZEE WA ZAMANI, UKIWA MJANJA KUCHAPIWA NI SIRI YA NDANI" kwa watu ambao hamjui tafsiri ya neno kuchapiwa hapo alimaanisha kwa uliyeoa kama ni mjanja mke wako akilala na mwanaume hiyo inabidi iwe siri yako. Hili ni fundisho potofu, maana Yesu alisema tunaruhusiwa kumuacha mke wako endapo umemfumania, lakini pia tukija katika sheria ya Mungu (Torati) inaonyesha wazi kuwa kuchapiwa ni laana na sio ujanja kama anavyosema Rich Mavoko. Ngoja ninukuu mstari huu kisha tumalizie somo, (
Kumbukumbu la Torati 28:30 Utaposa mke na mume mwingine atalala naye; utajenga nyumba usiikae; utapanda mizabibu usitumie matunda yake) Hizo ni miongoni mwa laana chache alizoahidiwa mtu ambae hatazishika amri za Mungu wala kuisikia sauti ya Mungu na kufuata maelekezo. Hivyo mimi namshauri Rich Mavoko na wenzake kuwa wanapotaka kuongelea swala lolote linalohusu ndoa au mahusiano ni vyema wakatutafuta kaka zao tukahariri mistari yao ili nyimbo zao zinapotoka ziwe nyimbo za maadili mbele ya jamii..
|
Msanii wa Bongo Fleva Rich Mavovo akiwa katika pozi |
|
Mtume wa Karne ya 21 Bashando akiwa anazungumza na wananchi |
No comments:
Post a Comment