Saturday, April 4, 2015

Shigongo aahidi kutoa vitabu 100 bure kwa watu mia moja wa kwanza watakaoudhuria

Kesho Grolious Worship Team watakuwa na tamasha litakalofanyika katika ukumbi uliopo katika sheli ya Victorious. Katika tamasha hilo lililoambatana na somo kutoka kwa mkufunzi mkubwa Tanzania Erick Shigongo hakutakuwa na gharama zozote za kiingilio ila zaidi ni watu mia moja watakaowahi watapewa nakala za vitabu mia moja bure. Mmoja wa viongozi wa kundi hilo Emmanuel Mabisa ameongea na Blog yetu na kusema wameamua kuandaa tamasha hilo ili kutoa elimu na kumfundisha mtanzania atakaehudhuria pale mambo muhimu yanayohusiana na maisha yake. Hivyo amewaomba wadau wote msikose kwasababu kutakuwa na burudani za kila aina kama vile mkali wa stand up comedy Mc Pilipili na waimbaji wengine. Lakini zaidi tutacheza na kuimba na tutaabudu ili kuzidi kujiimarisha kiroho.
Wote mnakaribishwa..

No comments:

Post a Comment