Wednesday, April 1, 2015

UKWELI KUHUSU HALI ILIYOMPELEKEA ASKOFU GWAJIMA KUZIMIA NA KUPOTEZA FAHAMU WAKATI AKIWA ANAFANYIWA MAHOJIANO NA POLISI.
 Swala la Askofu Gwajima limekuwa ni gumzo ndani ya jiji la Dar es Salaam na Tanzania kwa ujumla. Kila mtu amekuwa akizungumza jambo lake huku wengine wakizungumza hata yale wasiyokuwa na uhakika nayo. Hali hii imesababisha nifunguke na kuuliza majibu yatakayokupelekea kuhisi au kupata majibu ya jumla kuhusiana na gumzo hili lililozua utata na kuzidi kuwaacha watanzania katika hali ya sintofahamu. Hebu katika hali ya kawaida wewe jiulize, Askofu Gwajima alizungumza maneno makali ya kumkemea Kadinali Pengo ambapo polisi walimuita na kumuhoji, lakini alipofika alianguka na kupoteza fahamu kisha akakimbizwa katika hospitali ya TMJ akiwa mahututi, ameugua huko kwa takribani siku tatu na mwisho wa siku ametolewa huko akiwa hata hawezi kutembea, kama ni presha ilimpata je, ni presha gani hiyo ambayo imemsababisha hata baada ya  kupewa discharge hospital lakini ameondoka huku hawezi kutembea? Ni kitu gani kimesababisha miguu yake iishiwe nguvu? Ni kwanini Pengo asamehe lakini polisi washupalie kesi hiyo kupitia mtu mwenye majina matatu ya kiislam, fikiria hili kwa makini sana, mwisho wa siku utapata kitu kizito sana..

No comments:

Post a Comment