KAMANDA WA NYIMBO ZA INJILI APEWA SHAVU NA SHIGONGO KATIKA SEMINA YA UJASIRIAMALI
Mwanamuziki wa nyimbo za injili kwa mahadhi ya kizazi kipya Apostle Bashando amepata muariko wa kuimba katika semina kubwa ya wajasiriamali iliyoandaliwa na mkurugenzi wa Global Publisher. Semina hiyo itakayofanyika kwenye viwanja vya tandare kuanzia tarehe 1 April hadi Tarehe 4 April huku ikihusisha waimbaji mbalimbali kama vile H-Baba, Kala Jeremiah, Apostle Mashando, Pah One, Diamond plutnum, na wengine wengi itakuwa ni semina ya nguvu ambayo italeta mabadiriko makubwa kwa wakazi wa tandare na wengine wote watakaoihudhuria. Muda wa semina ni kuanzia saa nane mchana hadi saa kumi na mbili jioni ambapo wazungumzaji ni watu waliofanikiwa kutokea katika maisha ya chini hadi sasa ni matajiri wakubwa na wenye heshima hapa nchini, miongoni mwao ni Erick Shigongo na James Mwang'amba.
Usipange kukosa..
No comments:
Post a Comment