Saturday, April 4, 2015

Mchungaji Peter Sombasomba na Kampeni yake ya "Injili ni moto usiozimika, shetani kaa kimya" Anaendelea kuifanya kazi ya Bwana.


Katika shamba la BWANA kuna majembe ya aina nyingi na kila jembe linalima kutokana na uwezo wake.
Hakuna aliyebora zaidi ya mwenzake wala hakuna aliye duni zaidi ya mwingine bali kila mmoja anafanya kwa sehemu kwa kadiri ya Neema aliyokirimiwa na Mungu. Mchungaji Peter Sombasomba ni miongoni mwa watumishi mahiri ambao wanamtumikia Mungu katika viwango alivyomjalia. Juhudi na nidhamu ndiyo inayomuwezesha kuvuka mipaka ya Tanzania na kuingia hadi nnje ya Tanzania kwa ajili ya kuitangaza kazi ya BWANA. Mchungaji Peter Sombasomba ni Muhubiri na pia ni muimbaji wa nyimbo za injili katika mahadhi ya kizazi kipya (Hip Hop). Ana album nzima kwa sasa ambapo miongoni mwa nyimbo kali sana alizo nazo ni wimbo mmoja unaoitwa "Mambo yako kwa Yesu" kwakweli nyimbo hii ni nzuri sana na imekuwa nyimbo inayokubalika sana na vijana kila anaposimama kuimba. Mbali na uimbaji pia ana Kampeni inayoitwa injili ni Moto usiozimika, ambapo ndani ya kampeni hiyo anashirikiana na watumishi wengi akiwemo Alfred Funda maarufu kama Punda wa Yesu, George Yusufu na wengine wengi.. Kwa sasa Mchungaji Sombasomba yuko katika ziara yake ya kutangaza kampeni hiyo Ya injili ni moto usiozimika, ambapo nia na madhumuni makubwa ni kuhubiri zaidi na kuwaleta watu kwa Yesu, bila kukata tamaa wala kujari mazingira ni magumu.
Kwa sasa Mchungaji sombasomba anaendelea na kazi ya BWANA, Baada ya kumaliza mkutano wa Injili jijini mwanza na katika visiwa vya ukelewe sasa amepumzika kidogo hapa Dar es salaam na kukusanya nguvu, jumatatu anaanza tena ziara ya kuhubiri katika mkoa wa Dodoma.
Tukiwakama wakristo ni vyema kuwasuport watumishi kama hawa ili kuungana nao katika baraka zote za kuifikisha injili ya Kristo. Kama unaguswa kumsuport kifedha, au kumtia moyo wasiliana nae Mchungaji Sombasomba kwa namba 0716 851
970

No comments:

Post a Comment