Monday, April 6, 2015

MADAI YA UKAWA KABLA YA UCHAGUZI MKUU

Kufuatia uamuzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuahirisha Kura ya Maoni ya Katiba inayopendekezwa, viongozi wa UKAWA wameanza rasmi kuishinikiza Serikali kuiboresha Katiba ya sasa ili kuondoa mvutano katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba.

Mwenyekiti mwenza wa umoja huo, James Mbatia amesema kuwa kuna mambo manne ambayo yanadaiwa na UKAWA ambayo ni ushindi wa urais kuamuliwa kwa asilimia zaidi ya 50, mgombea binafsi katika nafasi za udiwani, ubunge na urais, tume huru ya uchaguzi na urais kupingwa mahakamani.

Mbatia amesema maboresho haya yaliafikiwa katika mkutano uliofanyika tarehe 8-Septemba-2014 kati ya Rais Jakaya Kikwete na vyama vya siasa chini ya Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD).

No comments:

Post a Comment