Friday, April 24, 2015

KUTANA NA KIJANA MOSES N NDOMBA KIJANA ALIYEKITAMBUA KIPAJI CHAKE NA HIVI SASA ANAISHI MAISHA MAZURI KUPITIA HICHO.

Anajulikana kwa jina la Moses Ndomba, mwenyeji wa Songea Ruvuma, ambae tangu akiwa shule ya msingi alipenda sana kujihusisha na michezo ya sarakasi. Mwanzoni alipenda kuifanya michezo hiyo kama sehemu ya kujifurahisha huku akiwa hana mikakati yeyote ya kukiendeleza kipaji chake, lakini alipokuwa akionekana anaruka sarakasi mbele za watu, wengi walimsifia na kumtia moyo kuwa anaweza wakiwemo waalimu wake wa shule ya msingi. Aliendelea na elimu yake ya msingi huko mkoani Songea ambapo pia katika maonyesho ya shuleni alishiriki michezo ya sarakasi. Alipofika darasa la sita kaka yake ambae walikuwa wakishirikiana kwenye michezo alimshauri  wahame kutoka songea na kuja dar ambapo kuna fursa kubwa ya kuendeleza vipaji vyao, kweli Moses na kaka yake walihama kutoka songea na kuja dar es salaam ambapo alimalizia elimu yake ya msingi katika shule ya buguruni A. Baada ya kumaliza elimu yake aliendelea na sanaa yake huku ikizidi kumtambulisha kwa watu mbalimbali na kumfanya apate miariko kadha wa kadha katika harusi na sehemu mbalimbali, mwisho wa siku wakajitokeza watu wa kumdhamini na hatimaye sanaa ya sarakasi ikawa ajira kwake, ya kumuendeshea maisha na kumpa mahitaji ya kila siku. Mwaka jana mwishoni Mungu alimfungulia mlango wa kupata mkataba wa kufanya kazi India kwa mwaka mzima ambapo sasa ameshatimiza miezi minne. Moses anamshukuru sana Mungu kwa hatua hii aliyopiga ambapo anasema ameanza kuona dalili kubwa za mafanikio kupitia sanaa yake, ambapo hadi sasa tayari anamiliki viwanja kadhaa Dae es Salaam na Ruvuma, na mbali na hayo anaamini mambo makubwa sana yataendelea kumtokea maishani mwake. Habari njema ni kwamba Moses ameokoka na anampenda Yesu, na ndoto zake ni kumtangaza Kristo kupitia sanaa yake popote pale anapopata nafasi.. Blog ya makamanda inamtakia mafanikio zaidi Mr Mosses Ndomba

Add caption




No comments:

Post a Comment