WATU WENGI WAMEKUWA NA MASWALI MENGI SANA KUHUSIANA NA HII HATUA YA UCHAGUZI MKUU TUNAOUELEKEA, WENGI WAMEKUWA WAKITABIRI MABAYA JUU YA NCHI YETU HUKU WAKIJARIBU KULINGANISHA HALI YA KISIASA ILIVYO KWA SASA HASWA WAKITOLEA MFANO RAIA WALIVYOKUWA NA MISIMAMO KATIKA KUDAI HAKI ZAO HASWA WALIVYOFANYA KATIKA UCHAGUZI WA WATENDAJI MWAKA HUU.
Kauri ya baadhi ya wabunge zimekuwa zikileta mashaka sana haswa ukizingatia wengi wamekuwa hawana nidhamu ya uoga tena juu ya serikali na jeshi la polisi tofauti na ilivyokuwa zamani, hizo ni dalili tosha za watu wenye upeo mdogo kusema nchii hii inakwwenda kuingia katika mapigano ya kisiasa. Ila ukweli utabakia pale pale kwamba nchi hii haiwezi kuingia kwenye mapigano kirahisi hivyo, amani tuliyo nayo ni zawadi tuliyopewa na Mungu, na Mungu ndio wa kuiondoa endapo akitaka kufanya hivyo, kuhusu dalili zote zinazojitokeza sasa hivi zile hatuziiti kama dalili za amani yetu kupotea bali ule ni ukomavu wa kisiasa ambao ni dalili nzuri kwa wapinzani na vijana wanaotaka mabadiriko katika nchi yao, vijana wa kisasa hatufikirii kupigana kwa bunduki ila tunaamini kura yetu ndio risasi pekee inayoweza kumuangusha tusiemtaka na kumuinua yule tunaemtaka. Hayo mambo ya kupishana kwa viswahili na kutoleaana maneno makali baina ya mbunge na mbunge hiyo ni hali ya kawaida sana kwenye siasa ambayo hata kwa wenzetu inatokea tena na zaidi ya hapo hadi wao wanafikia hatua ya kupigana makonde. Watanzania wenzangu naomba tuondoe hofu na tuondoe kabisa mtazamo wa kusema mabavu au kumwaga damu ndio jawabu la kutupatia tunachokitaka bali ni vyema tujue kura yetu ndi siraha yetu ya mwisho ambayo inaweza kutupatia haki yetu, na tukijidanganya na kuingia kwenye mapigano ye wenyewe kwa wenyewe atakaenufaika ni mwingine kabisa wakati sisi tunachinjana. Hebu dhamilia leo kutumia kura yako ili kuleta mabadiriko unayoyataka.
No comments:
Post a Comment