Friday, April 3, 2015

Apostle Augustus Baraza Matibila Atoa baraka zake kwa blog ya Makamanda, na aahidi kutoa suport ya kutosha ili kuhakikisha injili inasonga mbele

Mtumishi wa Mungu Apostle Augustus  amesema yuko tayari kutoa suport kwa blog ya makamanda ambayo nia na madhumuni ya blog hii ni kufikisha habari za ukweli zinazolihusu kanisa. Baraza ambae ni raia wa kenya lakini kwa sasa ni mkazi wa Washington DC huko Marekani aelezea kuwa anabarikiwa sana na maono ya Makamanda na amekuwa akifuatilia mada nyingi na kubarikiwa nazo, huku akipokea msg toka kwa watu wengi wanaosema wanafurahishwa na mtandao wa Makamanda. Mtumishi huyo ambae ana muda mrefu sana ndani ya injili na ameshatumika katika huduma mbalimbali ikiwemo ya uimbaji, zama hizo za akina Faustine Munishi, Mzungu Four, Geor Davie Kasambale, amesema akiwa katika mijadara ya makamanda huwa anakumbuka sana huduma na jinsi Mungu alivyowatumia na anavyoendelea kuwatumia hadi leo. 'Nimekuwa na mzigo sana wa kufuatilia na kuonya watu ambao ninaona wana kitu ndani yao, hivyo hata katika mtandao mimi sio mzungumzaji sana lakini kwa upande wa Bashando nimekuwa nikisukumwa toka ndani kumshauri, kumuonya na kumtiamoyo pale anapofanya vizuri, alisema Apostle Baraza. Akiendelea kuongea alisema kuwa enzi zao walitumia sana haswa katika kuandika mapambio ambapo mapambio mengi sana ambayo yanatumika makanisani. Hayo ni baadhi ya maelezo ya mtumishi huyu ambayo yanajenga na pia yanafurahisha moyo.

2 comments:

  1. aPOSTLE, Your
    BLEST SERVICES TO THE WORLD IS ADMIRED, LOVED
    RESPECTED. THANK YOU FOR YOUR PRAY, CARE AND GOSPEL TEACHINGS AND YOUR SPIRITUAL MUSIC.

    ReplyDelete
  2. from your musician, counselor. Sincerely submitted
    continue to let the Lord God lead and guide you.
    M Beverly Hunter

    ReplyDelete