Tuesday, April 28, 2015
Friday, April 24, 2015
KUTANA NA KIJANA MOSES N NDOMBA KIJANA ALIYEKITAMBUA KIPAJI CHAKE NA HIVI SASA ANAISHI MAISHA MAZURI KUPITIA HICHO.
Anajulikana kwa jina la Moses Ndomba, mwenyeji wa Songea Ruvuma, ambae tangu akiwa shule ya msingi alipenda sana kujihusisha na michezo ya sarakasi. Mwanzoni alipenda kuifanya michezo hiyo kama sehemu ya kujifurahisha huku akiwa hana mikakati yeyote ya kukiendeleza kipaji chake, lakini alipokuwa akionekana anaruka sarakasi mbele za watu, wengi walimsifia na kumtia moyo kuwa anaweza wakiwemo waalimu wake wa shule ya msingi. Aliendelea na elimu yake ya msingi huko mkoani Songea ambapo pia katika maonyesho ya shuleni alishiriki michezo ya sarakasi. Alipofika darasa la sita kaka yake ambae walikuwa wakishirikiana kwenye michezo alimshauri wahame kutoka songea na kuja dar ambapo kuna fursa kubwa ya kuendeleza vipaji vyao, kweli Moses na kaka yake walihama kutoka songea na kuja dar es salaam ambapo alimalizia elimu yake ya msingi katika shule ya buguruni A. Baada ya kumaliza elimu yake aliendelea na sanaa yake huku ikizidi kumtambulisha kwa watu mbalimbali na kumfanya apate miariko kadha wa kadha katika harusi na sehemu mbalimbali, mwisho wa siku wakajitokeza watu wa kumdhamini na hatimaye sanaa ya sarakasi ikawa ajira kwake, ya kumuendeshea maisha na kumpa mahitaji ya kila siku. Mwaka jana mwishoni Mungu alimfungulia mlango wa kupata mkataba wa kufanya kazi India kwa mwaka mzima ambapo sasa ameshatimiza miezi minne. Moses anamshukuru sana Mungu kwa hatua hii aliyopiga ambapo anasema ameanza kuona dalili kubwa za mafanikio kupitia sanaa yake, ambapo hadi sasa tayari anamiliki viwanja kadhaa Dae es Salaam na Ruvuma, na mbali na hayo anaamini mambo makubwa sana yataendelea kumtokea maishani mwake. Habari njema ni kwamba Moses ameokoka na anampenda Yesu, na ndoto zake ni kumtangaza Kristo kupitia sanaa yake popote pale anapopata nafasi.. Blog ya makamanda inamtakia mafanikio zaidi Mr Mosses Ndomba
Add caption |
Wednesday, April 22, 2015
ZITAMBUE AINA TATU ZA WANADAMU NI SOMO LINALOFUNDISHWA NA MTUMISHI WA MUNGU MCHUNGAJI PASCAL LINUS MJILI, JITAHIDI USOME HADI MWISHO ILI UJITAMBUE UKO KWENYE KUNDI GANI
SOMO: AINA TATU 3 ZA WANADAM.
Ktk ulimwengu huu tuonaishi kumejaa Wanadam wenye mitazmo mbalimbali tamaduni na desturi tofauti. Ktk some hili nitazungumzia aina Tatu za Wanadam ambazo zitatusaidia kujitasmini na kujitambua kuwa uko ktk kundi au group gani. Natumaini kila mmoja wetu atapa fursa ya kujifunza ktk some hili.
1. MWANADA WA ASILI(Natural person)
Ni mtu ambaye huishi kwa kufuata mifumo ya maisha ya kidunia. Ni mtu ambaye hajaokoka (ungenerated person) Ni mtu asiyemjua Mungu, hana ushirika wala mawasiliano na Mungu. Ni mtu aliyekufa kiroho, (spiritual dead person ) he is under control of Satan. Things of God are foolishness to him. Hijivunia dini zilizoanzishwa na wanadam badala ya wokovu ulioletwa na Yesu KRISTO. Fikra na akili zao zimetiwa Giza, mioyo yao imekufa ganzi, wana mioyo migumu wamefakana na uzima wa Mungu (Efeso 4:18-19) Hekima yao ni upuuzi kwa Mungu na Hekima ya Mungu ni upuuzi kwao.
2.MTU WA KIROHO (spiritual person)
Ni mtu alilye okoka (regenerated person) amezaliwa mara ya pili. Mungu Baba mwana na Roho mtakatifu wanakaa ndani yake. Ana ushirika na mawasiliano na Mungu wa milele. They can understand spiritual things because they are no longer natural person, they are converted from natural to spiritual. Wako tayari kutii na kufuata maelekezo ya Mungu, Neno na watumishi wake. Niwanyenyekevu..........
Niwatakatifu wameoshwa dhambi na ndiyo ambao Mungu wa mbinguni anajivunia (Zaburi 16;3) Ni watu ambao wana sifa kuu 2
(A) Makuhani
(B) Wafalme Ufunuo 5:10. Ni makuhani juu ya maisha yao wenyewe maanake waweza kujiwakilisha (kujiombea) kwa Mungu kwa njia ya damu ya Yesu KRISTO. Pia wanauwezo wa kuwaombea wengine na wakasikilizwa (YOHANA 9:31
Ni watawala juu ya nchi, uchumi, biashara makampuni mf ni Yusufu aliye tawala misri. Wana nguvu juu ya Mapepo majina uchawi. Wana amri juu Magonjwa yote na udhaifu wa kila aina.
3. MTU WA MWILINI (Carnal person )
Ni mtu aliye zaliwa mara ya pili ila hajakuwa kiroho, tabia za mwili huchukuwa sehemu kubwa ya maisha yake (1Kor.3:1-3) watu hawa wapo makanisa ya watu waliozaliwa mara ya pili ila tabia zao ni za kimwili mf. Mashindano, chuki, fitina, wivu na mengine kama hayo. Ni watu ambao wana moyo mapacha yaani moyo uliogawanyika.
Wanapenda vya dunia na vya Yesu pia wanavitaka . (they are mr&mrs both ways. They are still dancing and controls awith the devil. They always compromising with the world. Eliya alwahi kukutana na aina hii ya wayahudi ambao mioyo yao ilimwabudu Baali na bado wakitaka kuitwa watu wa Mungu wa Israel. Eliya aliwambia mtasitasita kati ya mawazo na njia mbili hata lini!? Baali akiwa ni Mungu mfuateni au BWANA akiwa ndiye Mungu haya mfuateni yeye.
Natumaini mpendwa umejifunza na kujitathimini uko ktk kundi gani ktk haya matatu. Fanya maamuzi ya kuwa ktk kundi la mtu wa kiroho.
Kama uko ktk kundi la mtu wa ASILI basi tubu dhambi na kuziacha mwamini Yesu ili uzaliwe mara ya pili, nawe utakuwa mtu wa kiroho.
Kama umeokoka lakini bado unatabia za kimwili Yesu KRISTO unampenda lakini duniani nako unapenda fanya maamuzi leo ya kuwa mtu wa kiroho. Huwezi kupanda mabasi au ndege mbili ktk safari moja. Tumia basi moja au ndege moja kwa safari moja. Kwa maana mtu akiipenda dunia kumpenda Mungu hakumo ndani ya . yake. (1 YOHANA 2;15
Asanteni kwa kunisikiliza
Pastor Pascal Linus Mjili
Ktk ulimwengu huu tuonaishi kumejaa Wanadam wenye mitazmo mbalimbali tamaduni na desturi tofauti. Ktk some hili nitazungumzia aina Tatu za Wanadam ambazo zitatusaidia kujitasmini na kujitambua kuwa uko ktk kundi au group gani. Natumaini kila mmoja wetu atapa fursa ya kujifunza ktk some hili.
1. MWANADA WA ASILI(Natural person)
Ni mtu ambaye huishi kwa kufuata mifumo ya maisha ya kidunia. Ni mtu ambaye hajaokoka (ungenerated person) Ni mtu asiyemjua Mungu, hana ushirika wala mawasiliano na Mungu. Ni mtu aliyekufa kiroho, (spiritual dead person ) he is under control of Satan. Things of God are foolishness to him. Hijivunia dini zilizoanzishwa na wanadam badala ya wokovu ulioletwa na Yesu KRISTO. Fikra na akili zao zimetiwa Giza, mioyo yao imekufa ganzi, wana mioyo migumu wamefakana na uzima wa Mungu (Efeso 4:18-19) Hekima yao ni upuuzi kwa Mungu na Hekima ya Mungu ni upuuzi kwao.
2.MTU WA KIROHO (spiritual person)
Ni mtu alilye okoka (regenerated person) amezaliwa mara ya pili. Mungu Baba mwana na Roho mtakatifu wanakaa ndani yake. Ana ushirika na mawasiliano na Mungu wa milele. They can understand spiritual things because they are no longer natural person, they are converted from natural to spiritual. Wako tayari kutii na kufuata maelekezo ya Mungu, Neno na watumishi wake. Niwanyenyekevu..........
Niwatakatifu wameoshwa dhambi na ndiyo ambao Mungu wa mbinguni anajivunia (Zaburi 16;3) Ni watu ambao wana sifa kuu 2
(A) Makuhani
(B) Wafalme Ufunuo 5:10. Ni makuhani juu ya maisha yao wenyewe maanake waweza kujiwakilisha (kujiombea) kwa Mungu kwa njia ya damu ya Yesu KRISTO. Pia wanauwezo wa kuwaombea wengine na wakasikilizwa (YOHANA 9:31
Ni watawala juu ya nchi, uchumi, biashara makampuni mf ni Yusufu aliye tawala misri. Wana nguvu juu ya Mapepo majina uchawi. Wana amri juu Magonjwa yote na udhaifu wa kila aina.
3. MTU WA MWILINI (Carnal person )
Ni mtu aliye zaliwa mara ya pili ila hajakuwa kiroho, tabia za mwili huchukuwa sehemu kubwa ya maisha yake (1Kor.3:1-3) watu hawa wapo makanisa ya watu waliozaliwa mara ya pili ila tabia zao ni za kimwili mf. Mashindano, chuki, fitina, wivu na mengine kama hayo. Ni watu ambao wana moyo mapacha yaani moyo uliogawanyika.
Wanapenda vya dunia na vya Yesu pia wanavitaka . (they are mr&mrs both ways. They are still dancing and controls awith the devil. They always compromising with the world. Eliya alwahi kukutana na aina hii ya wayahudi ambao mioyo yao ilimwabudu Baali na bado wakitaka kuitwa watu wa Mungu wa Israel. Eliya aliwambia mtasitasita kati ya mawazo na njia mbili hata lini!? Baali akiwa ni Mungu mfuateni au BWANA akiwa ndiye Mungu haya mfuateni yeye.
Natumaini mpendwa umejifunza na kujitathimini uko ktk kundi gani ktk haya matatu. Fanya maamuzi ya kuwa ktk kundi la mtu wa kiroho.
Kama uko ktk kundi la mtu wa ASILI basi tubu dhambi na kuziacha mwamini Yesu ili uzaliwe mara ya pili, nawe utakuwa mtu wa kiroho.
Kama umeokoka lakini bado unatabia za kimwili Yesu KRISTO unampenda lakini duniani nako unapenda fanya maamuzi leo ya kuwa mtu wa kiroho. Huwezi kupanda mabasi au ndege mbili ktk safari moja. Tumia basi moja au ndege moja kwa safari moja. Kwa maana mtu akiipenda dunia kumpenda Mungu hakumo ndani ya . yake. (1 YOHANA 2;15
Asanteni kwa kunisikiliza
Pastor Pascal Linus Mjili
Tuesday, April 21, 2015
MBUNGE WA MIKUMI ANAESUBILIA KUAPISHWA AUUNGA MKONO MTANDAO WA MAKAMANDA
Mwanamuziki mkongwe na icon of Bongo FlevaProfesor Jay amechangia sadaka ya ujenzi wa kanisa la Neema ya Kitume. Mwanamuziki huyo ambae kwasasa ametangaza nia ya kugombea ubunge baada ya wananchi wa Morogoro, jimbo la mikumi kumuhitaji ameongea na blog ya makamanda na kusema kuwa siku zote moyo wake huwa anahamisika sana kusaidia kazi yeyote inayomuhusu Mungu. "Niliona Tangazo lako facebook la kuchangisha pesa kwa ajili ya ujenzi wa kanisa na nikahamasika sana kutoa, naomba nitoe kidogo nilicho nacho pamoja na majukumu mengi niliyo nayo lakinini bora nishirikiane nanyikatika baraka hii ya kuijenga nyumba ya Mungu" Maneno hayo aliyasema huku akiambatanisha na pesa ambayo hakupenda sana itajwe kwa kudai kuwa sadaka siku zote ni siri na ametoa kwa ajili ya Mungu na wala sio kwa kutafuta ufahari. Profesa Jay ambae ana sifa ya kuubadilisha muziki wa bongo fleva toka kwenye kudharaulika hadi kugeuka na kuwa ajira kwa vijana wengi amesema hata huku bungeni ninapoelekea naamini Mungu ndio atakaenipa nafasi hiyo ambapo dalili zote nimeanza kuziona. Naomba muwe mnanitembelea hata baada ya kuingia bungeni maana mimi binafsi ninaamini sana katika ushauri wa watu mbalimbali hivyo msiache kunipa mawazo yengu.............. Blog ya makamanda inamshukuru sana Profesa Jay kwa mchango wake lakini pia kwa moyo wake wa kupenda kuwakaribisha wageni nyumbani kwake. Mungu akubariki....
Profesa Jay akisisitiza jambo katika maongezi yake na Kamanda Bashando |
Monday, April 20, 2015
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA
Simu: 255-22-2114 615, 211906-12
Barua pepe: nje@nje.go.tz
Barua pepe: gcu@nje.go.tz
Tovuti : www.foreign.go.tz
Nukushi: 255-22-2116600
20 KIVUKONI FRONT,
P.O. BOX 9000,
11466 DAR ES SALAAM,
Tanzania.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe, amesema leo kuwa hakuna Mtanzania kati ya watu wanane waliouwawa katika mashambulizi dhidi ya wageni huko Durban na Johannesburg nchini Afrika ya Kusini.
Mhe. Membe amewaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuwa taarifa zilizosambazwa na baadhi ya vyombo vya habari kwamba Watanzania watatu wameuwawa katika mashambulizii hayo siyo za kweli.
"Nimehakikishiwa na Waziri wa Usalama wa Afrika kusini, David Mahlobo, asubuhi hii kuwa hakuna Mtanzania kati ya watu wanane waliouwawa, ambao ni raia wa Ethiopia, Zimbabwe, Malawi na Swaziland," ametaarifu Mhe. Waziri.
Amesema serikali ina taarifa kuwa kuna Watanzania watatu waliofariki dunia nchini Afrika Kusini, lakini hawakuuwawa katika mashambulizi ya wenyeji dhidi ya wageni.
"Watanzania hao ni Rashidi Jumanne, ambaye imetaarifiwa alipigwa risasi katika tukio la ujambazi, kilometa 90 nje ya mji wa Durban; mfungwa Athumani China Mapepe, aliyeripotiwa kuchomwa kisu gerezani wakati wa vurugu za wafungwa, na Ali Heshima Mohamed, ambaye alifariki hospitalini kutokana na ugonjwa wa TB," alieleza Mhe. Membe.
Mwili wa marehemu Mohamed ulirejeshwa nchini jana kwa mazishi. Mhe. Waziri alitaarifu kuwa kuna Watanzania 23 katika kambi iliyotayarishwa na serikali ya Afrika Kusini huko Durban kuhudumia wageni wanaokimbia mashambulizi hayo ya wenyeji, na kuwa utaratibu unafanywa kuwarejesha nyumbani raia 21 walioomba. "Wawili wamesema hawako tayari kurudi."
Mhe. Membe amesema taarifa ya serikali ya Afrika Kusini inaonyesha kuwa hali ya utulivu imerejea Durban na Johannesburg katika saa 48 zilizopita kutokana na juhudi za Rais Jacob Zuma na kamati maalum ya mawaziri aliyoiteua kushughulikia mashambulizi hayo.
Mapema jana, Mhe. Membe alimwita Balozi wa Afrika Kusini nchini Tanzania, Mhe. Thamsanqa Dennis Mseleku, na kuelezea kukerwa kwa serikali na mauaji ya wageni na akataka hatua madhubuti zichukuliwe kuhakikisha usalama wa Watanzania nchini Afrika Kusini.
Alisema Tanzania inaunga mkono taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe, ambayo imelaani vikali mashambulizi ya Waafrika kutoka nje ya Afrika Kusini. Hata hivyo, Rais Mugabe, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU), amesifia hatua zinazochukuliwa na serikali ya Afrika Kusini kukomesha mashambulizi hayo na kurejesha utulivu.
Mhe. Membe aliwataka Watanzania waishio Afrika Kusini na kwingineko nje ya nchi, kujitambulisha kwenye balozi zetu ili iwe rahisi kufuatilia usalama wao na kuwasaidia pale yatokeapo majanga.
"Hatuna takwimu sahihi za idadi ya Watanzania waishio Afrika kusini kwa sababu wengi wao wamekwenda huko kwa njia za panya," alisema. Inakadiriwa kuna Watanzania 10,000 waishio Johannesburg na Durban.
Akijibu swali la mwandishi wa habari, Mhe. Membe alisema Tanzania inapaswa kutumia utajiri mkubwa wa gesi asilia ilionao ili kuendeleza viwanda vidogo, vya kati na vikubwa vitakavyotengeneza ajira za kuvutia kwa vijana ili wasikimbilie nchi za nje na kuhatarisha maisha yao.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Dar es Salaam
20 Aprili 2015.
Sunday, April 19, 2015
KWAYA YA BUGANDO YASHAURIWA KUWATEMA WANAKWAYA WANAOILETEA SKENDO KWA TABIA ZAO ZA KIPAGANI
Kwaya ya bugando ni kwaya kubwa sana hapa nchini, na ni kwaya iliyopata kibari sana kwa mzee wetu Hayati Moses Kulola. Kila mkutano ambao Askofu Kulola alikwenda kuhudumu ni lazima angeambata na kwaya hii ambayo hata mimi niliposhuhudia mikutano miwili mitatu nilivutiwa sana na uimbaji wao pamoja na staha waliyokuwa nayo. Lakini sasa mambo ni tofauti kabisa, baada ya Askofu Kulola kumaliza kazi yake na kuondoka hivi sasa baadhi ya wanakwayawameota mapembe na kufichua makucha yao, chakushangaza ni watu ambao wameishi kwa Askofu Kulola na wengine kusomeshwa elimu za juu ingawa sio watoto wake wa kuzaa, ila leo hii wamebadirika na wakuwa wa kidigital zaidi. Baadhi ya watu wamekuwa wakikereka na tabia za baadhi ya wanakwaya haoambao wamehudumu kwa muda mrefu na kwaya hiyo, lakini wengie wameishia kuwa walevi na wauza bar, wengine wakiwa na lugha za chafu huku wakisakamwa na skendo za kugombea mabwana. Mmoja kati ya walalamikaji ambae ni jirani wa dada mmoja katika kwaya hiyo, amedai kuwa wapo wanakwaya waliomaanisha lakini pia wako ambao hawajamaanisha ila tuwamejishikiza kwenye injili huku wakingojea mambo yao yaende vizuri watupilie mbali maigizo ya wakovu wanayoyafanya.
Blog ya Makamanda inatoa ushauri kwa msimamizi na mlezi wa kwaya hiyo awe mkali sana kwa wote wanaoonyesha tabia za kuichafua kwaya ambayo inaheshimika sana, ikiwezekana hata awatimue na kubakia na watu waliomaanisha, maana kazi ya Mungu inahitaji kujikana..
Blog ya Makamanda inatoa ushauri kwa msimamizi na mlezi wa kwaya hiyo awe mkali sana kwa wote wanaoonyesha tabia za kuichafua kwaya ambayo inaheshimika sana, ikiwezekana hata awatimue na kubakia na watu waliomaanisha, maana kazi ya Mungu inahitaji kujikana..
Mwanakwaya wa Kwaya ya Bugando akiwa amevalia mavazi ambayo hatuna uhakika kama Askofu Kulola angeyaafiki enzi akiwa hai |
Saturday, April 18, 2015
BISHOP NICKODEMUS SHABOKA NA ROSE SHABOKA MUNGU KAWAJAALIA MTOTO WA KIUME
Ni furaha ya ajabu kwa wanandoa wawili Nickodemus pamoja na mkewe Rose Shaboka baada ya Mungu kuwajalia mtoto wa kiume ambae wamempa jina la Prophet JM Shaboka. Baraka hii ilifanyika jana, Bishop Nickodemus amefurahishwa na ujio wa mtoto huyo. Mama wa Mtoto anaendelea vizuri.. Blog ya makamanda pamoja na makamanda wote tunatoa pongezi sana kwa wawili hao na tunazidi kumshukuru Mungu kwa kumsaidia Rose akajifungua salama..
Friday, April 17, 2015
BAADA YA VIPIMO VYA DAKTARI KUONYESHA KUWA EMMANUEL MBASHA HAKUBAKA, SASA MBASHA AIBUKA NA KIBAO KIPYA CHA KUUSHANGILIA USHINDI WA YESU DHIDI YA MAISHA YAKE
IJUE HUDUMA YA HUDUMA YA VICTORY FAITH ILIYOEGAMIA KATIKA IMANI YENYE MATENDO MAKUU YA KUUTUKUZA UFALME WA MUNGU
Apostle Mkalla ambae anaamini katika kuhubili injili ya kifalme amesema anapenda sana kuonyesha ubora katika kazi ya Mungu na ndio maana yeye hakubali kulala katika nyumba nzuri na kuiacha nyumba ya Mungu katika hali mbaya, nyonge na dhaifu. Japo kuna mapito mengi sana amepitia lakini katika yote ameshukuru sana Mke wake Glagys Mkalla ambae yeye amempa jina la The Machine, kwa jinsi anavyomuombea na kumtia moyo kwenye kazi ya Mungu, lakini pia kwa kuiongoza vyema team ya The Arrows ya kanisani hapo kwenye maombi. Apostle Mkalla amewashukuru sana pia na wachungaji wanaoongoza makanisa mengine ya Victory Faith hapa Tanzania na nnje ya Tanzania pamoja na waumini wote ambao wanatumika nae katika roho moja na nia moja. Kwa leo nimekuletea haya lakini bado nina mengi zaidi nitaendelea kukudokeza
Mama Mchungaji Gladys Mkalla |
Apostle Vincent Mkalla akiwa na Mke wake Glayds Mkalla madhabahuni |
Mfano wa jengo la kanisa ambalo Apostle Vincent aliutengeneza kwa ghalama zake baada ya Mungu kumuonyesha jengo hilo kwenye maono |
Waumini wa kanisa la Victory Faith wakiendelea na ibada |
Ramani ambayo Apostle aliichora baada ya kupata maono |
Picha ya kanisa la victory Faith |
Ujenzi wa kanisa ukiwa unaendelea |
Thursday, April 16, 2015
MWANAHARAKATI WA UKWELI BASHANDO AMUULIZA MASWALI MACHACHE FADHER NKWELA
Katika utoto wangu na hadi sasa ni kijana ninaeuelekea utu uzima nimekuwa nikisikia sana jina la Father Nkwella likitajwa na watu wengi, wakatoliki na na wakristo wasio wakatoliki. Wapo waliomuongelea kwa uzuri na wengine kumuongelea kwa ubaya, lakini katika miaka yote sijawahi kubahatia kumuona live Father Nkwella na hata kanisa lake sijui liko sehemu gani. Kwa bahati mbaya nilipata msiba siku ya ijumaa ambapo mazishi yalifanyika siku ya jumanne ya tar 12/April/2015 ambapo katika msiba huo Father Nkwella alihudhuria kwasababu marehemu alikuwa ni rafiki yake wa karibu sana na muumini wake. Baada ya mazishi kufanyika kuna mtu alinishtua kuwa yule unaemuona mbele yetu unamjua? Nikamjibu simfahamu, akaniambia kama umewahi kusikia mtumishi anaeitwa Father Nkwella ndio huyo. Aliponiambia hivyo nikasema siwezi kuondoka na kuishia kumuona kwa mbali ngoja nikamuombe angarau nipige nae picha, ingawa alikuwa amezungukwa na watu wengi lakini nilifanikiwa kupenya na kumfikia, nikakaa pembeni yake kwa muda wa dakika 10 na alipomaliza kuongea na watu ndio nikamumpa mkono na kumsalimia. Alipoitikia salamu yangu nikaonyesha jinsi nilivyofurahi kuonana nae na nikamuomba kupiga nae picha, hakuonyesha kusita akakubali mara moja, wakati tumemaliza kupiga picha niamuuliza kwa sauti ya chini chini, "Kanisa lako kwa chalinze liko wapi? Akanijibu hana tawi chalinze ila taratibu taratibu tu mambo yatakuwa. Nikamuuliza tena kwanini watu hasa jamii ya wakatoliki wenzake wanamuongelea vibaya na kufikia hadi hatua ya kuwanyima sakramenti waumini wake? Akanijibu, huduma yeyote ya kweli lazima ikutane na vita pamoja na kukataliwa na hiyo ndio tafsiri sahihi ya kukinywea kikombe cha Kristo. Swali la mwisho nikamuuliza je, yeye anatofauti gani na wakristo waliookoka? Na kwanini asijiite mchungaji yeye anajiita Father? Akanijibu eneo tulilopo sio sahihi sana kwa kujadiri mambo hayo ila nikihitaji kujua mengi ananikaribisha kanisani ubungo. Baada ya kunijibu hayo kwa njia ya hekima na upole kabisa niliona kweli nimuache kwanza mzee aendelee na majukumu mengine lakini nimepanga kumtafuta ili nimuulize mambo mengi sana kuhusiana na huduma yake.
Father Nkwella akiwa anapeana mkono wa salamu na Mjane wa Marehemu |
Father Nkwella akizungumza na Mjane wa Marehemu |
Father Nkwella akiwa amezungukwa na familia ya marehemu |
MTAKATIFU NA UZIDI KUJITAKASA MAANA KAMA IMANI NDIO IMEFIKIA HAPA BASI INAONYESHA ULE MWISHO UKO KARIBU
Wednesday, April 15, 2015
JINYAKULIE BARAKA ZAKO KWA KUCHANGIA UJENZI WA NYUMBA YA IBADA
Kanisa la Neema Ya Kitume. (A,M.G) lililopo tabata linanaendelea na shuguli ya ujenzi.. Kanisa hilo ambalo linasimamiwa na Apostle Bethania Simon liko katika uhitaji wa vifaa mbalimbali vya ujenzi ambavyo vitafanikisha kumalizika kwa kanisa hilo. Blog ya makamanda ilipozungumza na Apostle Bethania tulimuuliza ni hatua gani waliyoifikia kwenye ujenzi wa jengo hilo, Apostle Bethania alisema anashukuru kwasababu hadi hapo walipofika wameshapiga hatua, na sehemu iliyobakia ni ndogo sana ukilinganisha na walipotoka. "Kwa sasa tunahitaji mifuko 30 ya simenti pamoja na mabati 70, tunamshukuru Mungu kwa kutuinulia watu mbalimbali ambao wanajitokeza kuisuport kazi ya Mungu" alisema Apostle Bethania, akiendelea kuongea alitoa shukrani zake kwa mzee mmoja aliyemtaja kama MR SAMSON MAGOTI aliyeahidi kutoa mabati 60 kwa ajili ya ujenzi wa kanisa hilo, lakini amesema bado ana uhitaji wa mabati 70 maana ili jengo likamilike yanahitajika mabati 130. Blog ya makamanda inakuletea ombi hili na kukushauri uchangie kwa chochote ulicho nacho na Mungu wa mbinguni atakujaza na kukuongezea pale ulipopunguza.
Kwa uliyeguswa na kusuport kazi hii unaweza kutuma pesa yako kwa Mpesa 0755 259780 au tigopesa 0715 796667 Au kama unaweza kununua vifaa kwa jinsi vilivyo unaweza kuwasiliana na Apostle Bthania kwa namba hizo zote mbili...
Kwa uliyeguswa na kusuport kazi hii unaweza kutuma pesa yako kwa Mpesa 0755 259780 au tigopesa 0715 796667 Au kama unaweza kununua vifaa kwa jinsi vilivyo unaweza kuwasiliana na Apostle Bthania kwa namba hizo zote mbili...
Apostle Bethania Simon akisaidia kufanya kazi katika ujenzi wa nyumba ya BWANA |
Waumini wa kanisa la neema ya kitume wakiendelea na kazi ya ujenzi |
AJALI NYINGINE TENA YATOKEA NCHINI..
Monday, April 13, 2015
TAZAMA VIDEO YA WABUNGE WA KENYA WAKITWANGANA MANGUMI MAZITO MAZITO BAADA YA KUSHINDWA KUELEWANA
WATU WENGI WAMEKUWA NA MASWALI MENGI SANA KUHUSIANA NA HII HATUA YA UCHAGUZI MKUU TUNAOUELEKEA, WENGI WAMEKUWA WAKITABIRI MABAYA JUU YA NCHI YETU HUKU WAKIJARIBU KULINGANISHA HALI YA KISIASA ILIVYO KWA SASA HASWA WAKITOLEA MFANO RAIA WALIVYOKUWA NA MISIMAMO KATIKA KUDAI HAKI ZAO HASWA WALIVYOFANYA KATIKA UCHAGUZI WA WATENDAJI MWAKA HUU.
Kauri ya baadhi ya wabunge zimekuwa zikileta mashaka sana haswa ukizingatia wengi wamekuwa hawana nidhamu ya uoga tena juu ya serikali na jeshi la polisi tofauti na ilivyokuwa zamani, hizo ni dalili tosha za watu wenye upeo mdogo kusema nchii hii inakwwenda kuingia katika mapigano ya kisiasa. Ila ukweli utabakia pale pale kwamba nchi hii haiwezi kuingia kwenye mapigano kirahisi hivyo, amani tuliyo nayo ni zawadi tuliyopewa na Mungu, na Mungu ndio wa kuiondoa endapo akitaka kufanya hivyo, kuhusu dalili zote zinazojitokeza sasa hivi zile hatuziiti kama dalili za amani yetu kupotea bali ule ni ukomavu wa kisiasa ambao ni dalili nzuri kwa wapinzani na vijana wanaotaka mabadiriko katika nchi yao, vijana wa kisasa hatufikirii kupigana kwa bunduki ila tunaamini kura yetu ndio risasi pekee inayoweza kumuangusha tusiemtaka na kumuinua yule tunaemtaka. Hayo mambo ya kupishana kwa viswahili na kutoleaana maneno makali baina ya mbunge na mbunge hiyo ni hali ya kawaida sana kwenye siasa ambayo hata kwa wenzetu inatokea tena na zaidi ya hapo hadi wao wanafikia hatua ya kupigana makonde. Watanzania wenzangu naomba tuondoe hofu na tuondoe kabisa mtazamo wa kusema mabavu au kumwaga damu ndio jawabu la kutupatia tunachokitaka bali ni vyema tujue kura yetu ndi siraha yetu ya mwisho ambayo inaweza kutupatia haki yetu, na tukijidanganya na kuingia kwenye mapigano ye wenyewe kwa wenyewe atakaenufaika ni mwingine kabisa wakati sisi tunachinjana. Hebu dhamilia leo kutumia kura yako ili kuleta mabadiriko unayoyataka.
AJALI NYINGINE YA BASI LA PRINCES MUNA LINALOTOKA DAR KWENDA MWANZA
YALIYOJIRI ZANZIBAR, KIJANA AKUTWA AMEJINYONGA KATIKA HOTELI ALIYOKUWA AMEKODISHA CHUMBA
Kijana mmoja wa asili ya kiarabu alitoka Oman akakodi chumba hoteli moja
Zanzibar, akawa analewa tuu, sasa pale hoteli wakamuomba pesa za chumba
akawaambia angewapa asubuhi ya jana.
Wahudumu hiyo jana asubuhi wakaenda kumgongea ili alipe pesa ya chumba,
baada ya kugonga kwa muda mrefu wakaona hafungui ndipo walipoamua
kuvunja mlango na wakashangaa kukuta jamaa kaisha jinyonga kitambo.
Saturday, April 11, 2015
Friday, April 10, 2015
KUTANA NA MWANAKWAYA ALIYEGEUKIA KWENYE BIASHARA YA BIA, HIVI SASA ANAMILIKI BAR SINZA NA ANAKUNYWA ILE MBAYA
Dada mmoja aliyekuwa anaimba kwaya ya bugando iliyokuwa ikizunguka na Mzee Kulola enzi za uhai wake inasemekana amemuasi BWANA na kuanza kujishughulisha na shuguli za kuuza pombe. Dada huyu aliyekuwa ameokoka kabisa na amekulia kwa late Bishop Kulora EAGT.
Huko mwanza wazazi wake walikosa uwezo wa kumsomesha hivyo akasomeshwa
na Askofu kulora mpaka akapata Diploma ya Accounting chuo cha CBE
Mwanza, alikuwa ni muumini mzuri sana na mwimba kwaya ya Bugando iliyokuwa ikizunguka na Askofu Kulora ktk enzi za huduma yake. Chanzo cha habari kinasema binti huyu alikataa wachumba kama zaidi ya wanne walio okoka kisha akaja
kuolewa na mtu ambae hajaokoka lakini yuko vizuri kiuchumi, "yaani tangu aolewe haendi tena kanisani bali kazi yake ni kushinda kwenye bar ya mume wake huku anakunywa na kuuza bia.'' kilisema chanzo hicho.. Blog ya makamanda tuko kwenye maombi kumuombea dada yetu ili aweze kumrudia Mungu maana tunajua hilo ni jaribu ambalo mkono wa BWANA unaweza kumchomoa huko....
RICH MAVOKO AWEKWA KWENYE KIBANO KWA AJILI YA NENO LAKE LA "KUCHAPIWA NI SIRI YA NDANI"
Wapenzi wasomaji wa blog ya Makamanda naomba nichukue nafasi hii kuzungumza na mdogo wangu Rich Mavoko ambae ni muimbaji wa Bongo fleva, lengo langu sio kumponda bali nikumuweka sawa kama kaka ambae kwa maswala mengi nina upeo mkubwa sana zaidi yake. Mimi ni miongoni mwa watumishi wachache ambao sina tatizo na kusikiliza muziki wa aina yeyote, hivyo katika flash yangu nina baadhi ya nyimbo za bongo fleva ambazo huwa nazisikiliza, na kweli kabisa nazungumza, katika bongo fleva kuna wasanii ambao nawafuatilia sana na ninapenda kazi zao ingawa zina mapungufu, lakini huwa nikiwasikiliza naona kabisa wana nafasi ya kufanya vizuri na kuijenga jamii yetu endapo wakipata ushauri toka kwa watu makini kama mimi. Miongo mwa wasanii hao ni Christian Bella, Diamond Plutnum, Rich Mavoko, Rama Dee, na Profesor Jay. Kwakweli hawa watu nawakubali na ninawaombea kwa Mungu injili ipenye ndani yao. Ila katika kuwapenda na kuyaona mapungufu yao, naomba nitumie ukurasa huu ama blog hii kuwakosoa kila ninapopata nafasi. Leo nitaanza na Rich Mavoko na hawa wengine watafuatia siku nyingine. Huyu kijana Rich Mavoko ana wimbo wake mmoja unaitwa roho yangu, na katika verse ya wimbo huo kuna neno kalitumia linalosema "HAYA MANENO WALISEMA WAZEE WA ZAMANI, UKIWA MJANJA KUCHAPIWA NI SIRI YA NDANI" kwa watu ambao hamjui tafsiri ya neno kuchapiwa hapo alimaanisha kwa uliyeoa kama ni mjanja mke wako akilala na mwanaume hiyo inabidi iwe siri yako. Hili ni fundisho potofu, maana Yesu alisema tunaruhusiwa kumuacha mke wako endapo umemfumania, lakini pia tukija katika sheria ya Mungu (Torati) inaonyesha wazi kuwa kuchapiwa ni laana na sio ujanja kama anavyosema Rich Mavoko. Ngoja ninukuu mstari huu kisha tumalizie somo, (Kumbukumbu la Torati 28:30 Utaposa mke na mume mwingine atalala naye; utajenga nyumba usiikae; utapanda mizabibu usitumie matunda yake) Hizo ni miongoni mwa laana chache alizoahidiwa mtu ambae hatazishika amri za Mungu wala kuisikia sauti ya Mungu na kufuata maelekezo. Hivyo mimi namshauri Rich Mavoko na wenzake kuwa wanapotaka kuongelea swala lolote linalohusu ndoa au mahusiano ni vyema wakatutafuta kaka zao tukahariri mistari yao ili nyimbo zao zinapotoka ziwe nyimbo za maadili mbele ya jamii..
Msanii wa Bongo Fleva Rich Mavovo akiwa katika pozi |
Mtume wa Karne ya 21 Bashando akiwa anazungumza na wananchi |
Subscribe to:
Posts (Atom)