Mmoja wa waalimu katika semina hiyo ni Mwalimu Stephen Haule ambae amekuwa na sifa ya kuwa mfanyakazi bora katika kila sehemu anayokwenda kufanyia kazi. Amekuwa mwalimu wa secondary kwa takribani miaka kumi katika shule ya Tegeta secondary, na alianza katika ualimu katika ngazi ya kawaida tu, lakini kadiri siku zilivyozidi kwenda ndipo wakubwa waliziona juhudi zake na kuanza kumpandisha daraja taratibu, hadi anaondoka shuleni hapo na kuhamia katika ajira nyingine wanafunzi wa Tegeta secondary waligoma na wakasema wanamuhitaji mwalimu wao arudi, jambo lililofanya wakubwa wa shule hiyo wamuombe arudi hata kwa masharti ya kumuongezea mshahara anaoutaka ili tu wanafunzi wake wawe na amani.
Katika kazi nyingine aliyohamia aliingia kama mfanyakazi wa kawaida tu lakini kadiri siku zilivyozidi kwenda viongozi waliona juhudi zake na moyo wa kupenda kazi na wakaanza kumpandisha vyeo taratibu, hadi leo hii amefikia nafasi ya country manager katika kampuni ya Letshego Tanzania Limited. Anamuamini sana Mungu, lakini pia anaamini katika kufanya kazi kwa bidii na katika kuwasaidia wengine ili watimize ndoto zao. Kitu kikubwa ambacho hakipendi ni hapendi watu wasiojishughulisha na kuamini kila kitu kwao kuwa hakiwezekani, bali anapenda na pia anajitahidikwa kadiri anavyopata nafasi kumsababisha mtu aweze kusimama na kujisimamia maisha yake mwenyewe pasipo kuwa tegemezi wa mtu mwingine.
Ninayo mengi tu ya kumsimulia huyu mwalimu Haule ambae kwa sasa ni miongoni mwa viongozi wanaosimamia chama cha kusaidiana cha wafanyakazi wa tegeta CHAKUTE, na pia bado ni country manager wa kampuni ya Letshego Tanzania Limited, na pia ni mkufunzi wa mafunzo mbalimbali ya kazi pamoja na ujasiriamali. Binafsi huwa namshukuru na nitazidi kumshukuru kwasababu yeye pia ni mtu aliyeweka alama maishani kwangu, ukitaka kujua mengi kuhusu yeye hakikisha unatuhudhuria semina hii ambayo iko mbele yetu.
Mwalimu Stephen Haule alipokuwa katika ziara ya kikazi Africa ya kusini |
No comments:
Post a Comment