
Baba na mlezi wa huduma yangu ya Makamanda wa Yesu Apostle Vincent Mkalla ni miongoni mwa watumishi wa Mungu waliofanikiwa sana kiuchumi hapa Tanzania. Ninaposema amefanikiwa kiuchumi namaanisha kuwa ni tajiri sana kiasi kwamba hadi baadhi ya watu wenye upeo mdogo huwa wanamuita Freemason.
Juzi jumamosi mtumishi huyunalikuwa anabatiza waongofu wapya na kuzika utu wao wa kale, Mungu akampatia neema kubwa maana katika ubatizo huo alibeba watu katika Coaster 11 ambazo zote zilikuwa zimejaza watu.
Licha ya upako na mafanikio aliyo nayo lakini huyu baba ni mnyenyekevu sana, na mimi ninamiheshimu kwasababu keshapitia vita kubwa sana na Mungu akampigania hadi leo hii anaendelea na huduma. Kanisa lake liko Arusha maeneo ya Kijenge, Mwanama, linaitwa Victory Faith. Siku moja nikiwa naongea nae nilimuuliza ni nini siri ya mafanikio yake kiuchumi na kihuduma? Akanijibu kuwa ni uaminifu mbele za Mungu na kuisimamia kweli. Kisha akanipa shuhuda kuwa amewahi kupewa pesa kwa ajiri ya huduma fulani, ilikuwa ni kama shilingi million mbili hivi, na wakati huo hakuwa hata na nauri, tena yeye alikuwa anakaa Arusha na pesa hiyo alipewa wakati yuko moshi, ikambidi atembee kwa miguu toka Moshi hadi Arusha huku akiwa amezihifadhi hizo pesa za huduma bila kuchomoa hata senti tano. Na hiyo aliifanya ili kuutiisha mwili na kuufundisha moyo wake kuheshimu kila pato linalotokana na huduma ili aushinde moyo na matamanio ya uharibifu ndani ya huduma. Miaka mingi baadae Mungu akaja kumfanikisha sana kihuduma na kifedha, na pia akamfungulia milango mingi ya nnje, na kumpa marafiki wakubwa ambao ni watumishi Maarufu sana ulimwenguni. Siku moja Apostle Vincent Mkalla alihubiri kanisani hapo Victory Faith, Injili ikapenya sana mioyoni mwa watu, hadi washirika fulani matajiri mtu na mke wake wakaenda benki na kudroo shilingi million 15 Kisha wakaja kumkabidhi kama mbegu, huku wakidai kuwa ni Mungu amewaambia wampatie sadaka hiyo. Apostle Vincent Mkalla akaipokea ile pesa na kuihifadhi bila kuchomoa hata shilingi kumi. Baada ya mwezi wale washirika wakampigia simu na kumwambia kuwa mambo yao hayaendi vizuri na watoto wao wamerudishwa nyumbani baada ya kukosa ada ya shule. Apostle akawaita wale ndugu wakaenda kuonana, kisha akawauliza "Ni kwanini mumtolee Mungu alafu badala ya kubarikiwa nyinyi muingie kwenye matatizo? Wale watu wakakosa jibu, Kisha Apostle akawafundisha tofauti iliyopo kati ya kutoa kwa kusikia sauti ya Mungu na na kutoa kwa kufuata hisia baada ya kusikia Injili iliyochangamka. Baada ya hapo akawaonyesha zile pesa ambazo walizitoa, akachukua shilingi million tano na kumkabidhi baba yule kwa ajiri ya kwenda kuwalipia watoto ada, kisha baada ya hapo akamchukua kwenye gari wakaenda hadi benki na kuziingiza zile shilingi million kumi zilizobakia kwenye account yao. Ile familia ilishangazwa sana kwa uaminifu wa Apostle Vincent Mkalla na tangu siku hiyo hadi leo wamezidi kumuamini na kumuheshimu zaidi kama baba na mtumishi wa Mungu. Sasa kwa uaminifu wa namna hii kwanini Mungu asikubariki na kukuinua katika viwango vya hali ya juu!! Historia hii njema na mimi pia imeniongezea kitu katika utumishi wangu na kunifanya nimchukue mtumishi huyu kama mfano wa kuigwa. Ndiyo maana nimekushirikisha na wewe ili uweze kushiriki ushuhuda huu pamoja nami.
No comments:
Post a Comment