CHAKUTE ni chama cha kusaidiana cha wafanyakazi wa tegeta. Ofisi za chama hichi ziko tegeta. Asilimia kubwa ya wanachama wa chakute ni waalimu wa secondary ambao wengine wako kwenye ajira ya ualimu na wengine wako katika ajira nyingine tofauti na ualimu ingawa walishapita kwenye ualimu na kufanya vizuri. Wafanyakazi hawa walikaa chini na kubuni kitu ambacho kitakuwa ni msaada kwa jamii inayowazunguka na moja kati ya miradi waliamua kutumia taaluma yao ilikusaidia watanzania katika upande wa elimu. Bila shaka kwa waliosoma Tegeta miaka ya 1999 hadi 2006 watakuwa wanamjua vyema mwalimu Steven Haule ambae alikuwa ni mwalimu katika shule hiyo, huyu pia ni miongoni mwa wanachama wa CHAKUTE ambao wameamua kubuni kitu kitakachoweza kusaidia wengi ktika upande wa elimu hususani wale wasiokuwa na uwezo mkubwa kifedha au wale waliosoma na kushindwa kuendelea na masomo yao kwa sababu mbalimbali . Chakute wakishirikiana na shule ya One Nursery and Primary school sasa wanakuletea elimu bora kwa gharama nafuu. blog ya Makamanda ilipokuwa ikifanya mahojiano na wanachama hao, mmoja kati yao alisema "Malengo yetu makubwa katika chama hichi ni kusaidiana sisi kwa sisi lakini pia kusaidia jamii inayotuzunguka kama vile watoto yatima, wajane, pamoja na watanzania wengine ambao hawakubahatika kupata elimu bora kwa wakati. Na ili tuweze kutimiza malengo yetu tumeamua tuanze na shule hii ambayo ndio itakuwa msaada kwa wengi utakaowapa uhuru wa kujitegemea maana katika zama hizi hakuna urithi unaoweza kuwa bora kwa mwanadamu zaidi ya urithi wa kupata elimu, alisema mmoja kati ya wanachama wa chama cha CHAKUTE. Kazi kwako mama, baba, kaka na dada unaehitaji elimu bora au wewe ambae unahitaji mtoto wako, mdogo wako au ndugu yako apate elimu bora, nafasi ya kuchangamkia ndio hii. Njoo ufundishwe na waalimu wenye taaluma, uzoefu, pamoja na bidii katika kazi yako ili maisha yako yapate mwangaza. Shule hii ni shule inayotambuliwa kiserikli na ipo imesajiliwa kwa mujibu wa sheria. Karibuni sana. Mawasiliano yetu yapo kwenye bango hapo juu. | | |
|
No comments:
Post a Comment