Saturday, June 6, 2015

MCHUNGAJI GABRIEL ARUDI KUWASHUKURU MAKAMANDA BAADA YA MUNGU KUWATUMIA KUGUSA MAISHA YAKE KWA NAMNA MOJA AU NYINGINE

Mchungaji Gabriel Y Kalima ametoa shukrani zake za dhati kwa makamanda wa Yesu. Huyu ni Mchungaji ambae takribani mwezi mzima uliopita nilimleta mbele zenu na kuwaeleza juu ya uhitaji wake. Nakumbuka alikuwa anahitaji mtaji wa shilingi laki nne kwa ajili ya kufanya biashara ambayo ingemuwezesha kupata mahitaji yake ya kila siku, na pesa aliyokuwa anaihitaji ni shilingi laki nne tu. Namshukuru Mungu kwa ajili ya wote mliojitoa kwa kuongea maneno ya kutia moyo, lakini zaidi namshukuru sana Apostle Vincent Mkalla ambae aliitoa pesa hiyo yote na kunikabidhi kisha mimi nikamfikishia Mchungaji. Badala ya kufanya biashara ya mabanzi Mchungaji Gabriel ameamua kufanya biashara ya kununua nguo na kuziuza mkoani ambapo biashara hiyo ameikabidhi kwa mama Mchungaji na hivi sasa inaenda vizuri. Siku tano zilizopita Mchungaji Gabriel amekuja ofisini kwangu Chalinze na kunipa shukrani zake za dhati kwa niaba ya makamanda wote, na vilevile nikampa muariko wa kuhudhuria semina ya siku mbili ya makamanda ambayo itafanyika tarehe 22/23 Agosti 2015, Mchungaji Gabriel ameahidi kuwepo katika semina hiyo na amesema atatoa ushuhuda wa jinsi Mungu alivyomtendea kupitia huduma hii ya Makamanda Wa Yesu.
Mchungaji Gabriel Kalima akiwa namke wake.

No comments:

Post a Comment