Sunday, June 28, 2015

JINSI UAMINIFU UNAVYOWEZA KUKUJENGEA HESHIMA MBELE ZA MUNGU NA MBELE ZA WATU UNAOWATUMIKIA..



Baba na mlezi wa huduma yangu ya Makamanda wa Yesu Apostle Vincent Mkalla ni miongoni mwa watumishi wa Mungu waliofanikiwa sana kiuchumi hapa Tanzania. Ninaposema amefanikiwa kiuchumi namaanisha kuwa ni tajiri sana kiasi kwamba hadi baadhi ya watu wenye upeo mdogo huwa wanamuita Freemason. Juzi jumamosi mtumishi huyunalikuwa anabatiza waongofu wapya na kuzika utu wao wa kale, Mungu akampatia neema kubwa maana katika ubatizo huo alibeba watu katika Coaster 11 ambazo zote zilikuwa zimejaza watu. Licha ya upako na mafanikio aliyo nayo lakini huyu baba ni mnyenyekevu sana, na mimi ninamiheshimu kwasababu keshapitia vita kubwa sana na Mungu akampigania hadi leo hii anaendelea na huduma. Kanisa lake liko Arusha maeneo ya Kijenge, Mwanama, linaitwa Victory Faith. Siku moja nikiwa naongea nae nilimuuliza ni nini siri ya mafanikio yake kiuchumi na kihuduma? Akanijibu kuwa ni uaminifu mbele za Mungu na kuisimamia kweli. Kisha akanipa shuhuda kuwa amewahi kupewa pesa kwa ajiri ya huduma fulani, ilikuwa ni kama shilingi million mbili hivi, na wakati huo hakuwa hata na nauri, tena yeye alikuwa anakaa Arusha na pesa hiyo alipewa wakati yuko moshi, ikambidi atembee kwa miguu toka Moshi hadi Arusha huku akiwa amezihifadhi hizo pesa za huduma bila kuchomoa hata senti tano. Na hiyo aliifanya ili kuutiisha mwili na kuufundisha moyo wake kuheshimu kila pato linalotokana na huduma ili aushinde moyo na matamanio ya uharibifu ndani ya huduma. Miaka mingi baadae Mungu akaja kumfanikisha sana kihuduma na kifedha, na pia akamfungulia milango mingi ya nnje, na kumpa marafiki wakubwa ambao ni watumishi Maarufu sana ulimwenguni. Siku moja Apostle Vincent Mkalla alihubiri kanisani hapo Victory Faith, Injili ikapenya sana mioyoni mwa watu, hadi washirika fulani matajiri mtu na mke wake wakaenda benki na kudroo shilingi million 15 Kisha wakaja kumkabidhi kama mbegu, huku wakidai kuwa ni Mungu amewaambia wampatie sadaka hiyo. Apostle Vincent Mkalla akaipokea ile pesa na kuihifadhi bila kuchomoa hata shilingi kumi. Baada ya mwezi wale washirika wakampigia simu na kumwambia kuwa mambo yao hayaendi vizuri na watoto wao wamerudishwa nyumbani baada ya kukosa ada ya shule. Apostle akawaita wale ndugu wakaenda kuonana, kisha akawauliza "Ni kwanini mumtolee Mungu alafu badala ya kubarikiwa nyinyi muingie kwenye matatizo? Wale watu wakakosa jibu, Kisha Apostle akawafundisha tofauti iliyopo kati ya kutoa kwa kusikia sauti ya Mungu na na kutoa kwa kufuata hisia baada ya kusikia Injili iliyochangamka. Baada ya hapo akawaonyesha zile pesa ambazo walizitoa, akachukua shilingi million tano na kumkabidhi baba yule kwa ajiri ya kwenda kuwalipia watoto ada, kisha baada ya hapo akamchukua kwenye gari wakaenda hadi benki na kuziingiza zile shilingi million kumi zilizobakia kwenye account yao. Ile familia ilishangazwa sana kwa uaminifu wa Apostle Vincent Mkalla na tangu siku hiyo hadi leo wamezidi kumuamini na kumuheshimu zaidi kama baba na mtumishi wa Mungu. Sasa kwa uaminifu wa namna hii kwanini Mungu asikubariki na kukuinua katika viwango vya hali ya juu!! Historia hii njema na mimi pia imeniongezea kitu katika utumishi wangu na kunifanya nimchukue mtumishi huyu kama mfano wa kuigwa. Ndiyo maana nimekushirikisha na wewe ili uweze kushiriki ushuhuda huu pamoja nami.

Friday, June 26, 2015

HAUNA HAJA YA KUWAZA SANA KUHUSU ELIMU BORA, CHAMA CHA KUSAIDIANA CHA WAFANYAKAZI WA TEGETA(CHAKUTE) KIMEKUPATIA UFUMBUZI

CHAKUTE ni chama cha kusaidiana cha wafanyakazi wa tegeta. Ofisi za chama hichi ziko tegeta. Asilimia kubwa ya wanachama wa chakute ni waalimu wa secondary ambao wengine wako kwenye ajira ya ualimu na wengine wako katika ajira nyingine tofauti na ualimu ingawa walishapita kwenye ualimu na kufanya vizuri. Wafanyakazi hawa walikaa chini na kubuni kitu ambacho kitakuwa ni msaada kwa jamii inayowazunguka na moja kati ya miradi waliamua kutumia taaluma yao ilikusaidia watanzania katika upande wa elimu.  Bila shaka kwa waliosoma Tegeta miaka ya 1999 hadi 2006 watakuwa wanamjua vyema mwalimu Steven Haule ambae alikuwa ni mwalimu katika shule hiyo, huyu pia ni miongoni mwa wanachama wa CHAKUTE ambao wameamua kubuni kitu kitakachoweza kusaidia wengi ktika upande wa elimu hususani wale wasiokuwa na uwezo mkubwa kifedha au wale waliosoma na kushindwa kuendelea na masomo yao kwa sababu mbalimbali . Chakute wakishirikiana na shule ya One Nursery and Primary school sasa wanakuletea elimu bora kwa gharama nafuu. blog ya Makamanda ilipokuwa ikifanya mahojiano na wanachama hao, mmoja kati yao alisema "Malengo yetu makubwa katika chama hichi ni kusaidiana sisi kwa sisi lakini pia kusaidia jamii inayotuzunguka kama vile watoto yatima, wajane, pamoja na watanzania wengine ambao hawakubahatika kupata elimu bora kwa wakati. Na ili tuweze kutimiza malengo yetu tumeamua tuanze na shule hii ambayo ndio itakuwa msaada kwa wengi utakaowapa uhuru wa kujitegemea maana katika zama hizi hakuna urithi unaoweza kuwa bora kwa mwanadamu zaidi ya urithi wa kupata elimu, alisema mmoja kati ya wanachama wa chama cha CHAKUTE. Kazi kwako mama, baba, kaka na dada unaehitaji elimu bora au wewe ambae unahitaji mtoto wako, mdogo wako au ndugu yako apate elimu bora, nafasi ya kuchangamkia ndio hii. Njoo ufundishwe na waalimu wenye taaluma, uzoefu, pamoja na bidii katika kazi yako ili maisha yako yapate mwangaza. Shule hii ni shule inayotambuliwa kiserikli na ipo imesajiliwa kwa mujibu wa sheria. Karibuni sana. Mawasiliano yetu yapo kwenye bango hapo juu.  

Wednesday, June 17, 2015

TOKEA KWENYE KUSAFISHA CHOO CHA KANISA HADI KUWA MTUMISHI BILIONAIRE.

Waswahili walisema ukistaajabu ya filauni utashangazwa na ya Musa, ama kweli wanadamu huwa hawakosi majina katika kila hali unayoipitia, ukiwa mwembamba watakuita kimbaumbau, na ukiwa mnene watakuita manyama uzembe, ili mradi tu wakupe kero na usijisikie furaha katika hali unayoipitia. Nimeanza na kuzungumza hayo kwasababu ya historia na shuhuda nzitto ninayotaka kuwaletea.
Leo nakwenda kumzungumzia Founder wa huduma ya Victory Faith, yenye makao makuu yake Arusha maeneo ya Kijenge Mwanama, anaejulikana kama Baba wa washindi Apostle Vincent Mkalla. Huyu ni mtumishi ambae Mungu anamtumia sana katika kufundisha mambo yanayohusiana na laana na jinsi ya kuziepuka. 
Kwa mara ya kwanza nimesikia historia yake toka kwa wachungaji fulani ambao walimtambulisha kwangu kama Freemason mmoja hatari sana, na nilipotaka kujua ni kwa nini wanasema hivyo au ni kitu gani kinawapa uhakika kuwa huyu ni Freemason wengi walisema huyu ni mtumishi mwenye pesa na mafanikio makubwa sana na wao hawajui pesa hizo amezitoa wapi?? Hali hii ilinisababisha nimtafute mtumishi wa Mungu huyu na kutaka kujua kama kweli yeye ni freemason kama nilivyosikia ili nijue wanafanyajefanyaje huko kwa chama cha freemason?? Story niliyokutana nayo ni tofauti kidogo na ikanifanya nikae chini na kuwaletea ukweli wa mambo.
Huyu mtumishi ni mtoto wa kipekee wa kiume na wa mwisho kwa mzee Mkalla ambae alikufa wakati yeye akiwa na siku 22 tangu azaliwe.
Katika kukua kwake historia ya baba yake kufa na aligundua kuwa aliuwawa hali ile ilimjengea uchungu moyoni na akawa amepanga kuja kulipa kisasi kwa wale waliohusika katika kifo cha baba yake. Mbali na masomo aliyoyapata lakini piaa alitumia muda wake mwingi katika kufanya mazoezi na pia kujihusisha na michezo ya kung fu ambayo ilimuwezesha hadi kuvuka hadi boda za Tanzania na kwenda nchi mbalimbali kwa ajili ya mafunzo hayo, nchi kama vile urusi ambapo katika mchezo huo alifikia kiwango cha kutunukiwa mkanda mweusi. Hapo alikuwa ni mkristo lakini alikuwa hajaokoka na wala hajawa mtumishi bali alikuwa ni rastafari anaemiliki chuo cha karate alichokiita jina la scopion yaani nnge. 
Miaka ilienda baadae akaja kuokoka, na siku alipookoka ndani ya siku mbili alinyoa rasta zake na kuendelea na kuwa mshirika mtiifu katika kanisa na pia muhudhuriaji na muhudumu katika mikutano ya injili.Na kazi yake kubwa ilikuwa ni kusafisha vyoo vya kanisa na kuhakikisha ni visafi kila wakati, kazi hiyo haikuwa na malipo ilikuwa ni kazi yake ya kujitolea na baadhi ya waumini wa kanisani wakambatiza kwa jina la kebehi la bwana mavi. Mwaka 1996 akiwa tayari ameshakomaa kwenye wokovu ndio mwaka aliofunga safari kutoka moshi na kuingia katika jiji la Arusha akiwa kamamgeni, ambapo moja kwa moja akaenda kufanya kazi ya umisionary katika kijiji kimoja cha Kimnyaki huko Meru. Huko aliweza kukutana na watumishi wa Mungu mbalimbali wakiwemo akina Askofu Ngataiti na Askofu Lyzer wa kanisa la habari maalum ambao hivi sasa ni marehemu. 
Wakati huo Apostle Vincent Mkalla hakuwa ameoa, na alikuwa ni miongoni mwa watumishi maskini sana, ambapo alikuwa amepewa hifadhi katika nyumba moja ya udongo ajihifadhi kama mtumishi, na humo ndani ya nyumba hakuwa na kitanda wala godoro bali alikuwa amemwaga mchanga mwingi chini, na ametengeneza mbao kama ile chaga, na juu ya hizo mbao ndio alikuwa analala, huku shuka yake ikiwa ni ile mifuko ya visalfeti ambayo huwa anakuja huku tz ikiwa imebeba viatu vya mitumba na mto wake ulikuwa ni biblia. Mwaka 1997 watumishi walikaa chini na kukubaliana kupinga tohara za jadi kwa wamasai baada ya kugundua wale wamasai wenye asili ya kiarusha tohara zao huwa zinaambatana na mambo mabaya ambayo ni ibada za mizimu, kwa mfano kila tohara ya hao wamasai wa asili ya kiarusha kabla ya kutahiri vijana huwa wanamuita Laibon ambae ni mganga wa kienyeji anaekwenda kwenye milima ya meru na kufukua jiwe fulani kila baada ya miaka saba na kuweka wakfu tohara hiyo huku wakiwa wanaimba nyimbo zao. Na kuna mengine mengi mabaya ambayo watumishi wa Mungu waliyabaini na kuamua kupinga tohara hiyo ambapo baadhi ya vijana wa kimasai waliafiki kutoshiriki tohara hiyo na kutaka watairiwe lakini bila muongozo wa mganga wa kienyeji Laibon, wala pasipo kuimbiwa nyimbo za kiasiri. Apostle Vincent Mkalla na mzee wake wa kanisa anaejulikana kama Ayubu ambae hivi sasa ni Mchungaji waliafiki kuwatahiri vijana hao kama walivyodai, hivyo wakachukua pesa kama shilingi laki nne kasoro na kuanza safari ya usiku kwenda kijiji cha jirani ili kuwatahiri vijana hao, wakati huo alikuwa katika mfungo wa siku 62, njiani walikutana na majambazi ambapo vijana pamoja na mchungaji Ayubu walikimbia lakini kwasababu yeye alikuwa kwenye mfungo alijikuta anaanguka chini na wale majambazi wakamkamata na kumuwekea bunduki kichwani huku wakimlazimisha atoe hela, akiwa katika kuwasikiliza jinsi alivyokuwa mchovu kwa ajili ya mfungo na koti alilovaa alisikika jambazi mmoja akisema "Achana nae huyu mzee atakuwa hana hela" na hiyo ndiyo ikawa pona yake. Alipoamka hapo aliendelea na safari ambapo mbele ndipo alikutana tena na mzee wa kanisa pamoja na wale vijana ambao walikimbia, safari yao ya kwenda kwangariba ikaendelea. walifanikiwa kufika kwa ngariba mida ya saa saba usiku na kazi ya kutahiri wale vijana ikaendelea, maana vijana walikataa kutahiriwa kimira lakini vilevile walikataa kutahiriwa kwa ganzi. Baada ya tohara hiyo walirudi kijiji cha Kimyaki ili wawarudishe kila kijana nyumbani kwao kabla ya wazee wamji kugundua kama vijana hawajatahiriwa kimira. Wakati wanarudi walifika kwenye daraja moja ambapo vijana walishindwa kuvuka ikabidi Apostle Vincent na Mchungaji Ayubu waanze kumvusha mmoja baada ya mwingine katika daraja lile, jambo la kushangaza nyuki waliwavamia na kuanza kuwang'ata kwelikweli lakini Mungu akawasaidia wakavuka salama, na mida ya saa kumi kuelekea kumi na moja walifanikiwa kufika kijijini na kumrudisha kila kijana nyumbani kwao. Baada ya wiki moja tukio lile likavuja lakini haikujulikana moja kwa moja ni nani aliyewapeleka vijana wale kwenye tohara, maana katika tohara wamasai wanakuwaga na mtu anaeitwa mdhamini, yaani mtu anaemshikilia kijana wakati wa kutahiriwa, sasa vijana wale walikamatwa na kuanza kuteswa huku wakiulizwa ni nani alikuwa mdhamini wake lakini wao wakajibu kuwa waliegamia mti, ambapo gadhabu ya wamasai wale waliielekezea kwenye mti walioelekezwa na wakaenda kuung'oa. lakini baada ya mti walianza operation ya kushughulika na wachungaji, ambapo jumanne moja Apostle Vincent alikuwa kanisani akiwa ametangaza semina, alishangaa amevamia na watu zaidi ya mia saba pale kanisani ambapo walimpiga fimbo za kutosha na wakamvunja mguu, na kuna bibi mmoja aliyekuwa muumini katika kanisa hapo alipigwa fimbo hadi akafa. Tukio hilo lilikuwa baya sana kiasi kwamba wachungaji wengine ambao walikuwa ni wenyeji wa jamii ile walikimbia na kuacha makanisa yao, wengine walikimbilia Kenya, wengine Morogoro, wengine Dodoma, huku wengi wakidhania Apostle Vincent amefariki dunia. Na kumbe Mungu alimponya na shambulizi lile lakini habari zilifika hadi kwa mama yake kuwa ameshafariki. Baada ya tukio hilo alitibiwa na akafungwa pop na akaendelea kusimama kwenye semina huku akiwa na muogo mguuni. Yeye aliendelea kumtumikia Mungu katika eneo lile ambapo jambo hilo lilisababisha hata wamasai wa jamii ile wamuhesabu kama mchungaji shujaa. Na habari hiyo ilivuma hadi kutangazwa kwenye vyombo vya habari kama vile bbc na sauti ya ujermani, hivyo ikaleta promo ya kiaina pale kijijini na kufanya semina ipete mahudhurio makubwa. Mwaka 1998 Apostle Mkalla alipata mchumba na mwaka 1999 akaoa, baada ya kuoa alikuwa amezawadiwa vyombo vya ndani na na mazagazaga kibao kama mnavyojua mambo ya harusi, lakini Mungu akamwambia jambo na akamshirikisha mke wake wakakubaliana kuchukua vitu vyao vyote na kwenda kumbariki Mchungaji mmoja ambae alikuwa anapitia katika wakati mgumu na hakuwa na vyombo vya ndani, na wao wakabakia hawana chochote kisha wakaanza kumlilia Mungu. Kweli walipita katika wakati mgumu sana wa kukosa hadi chakula lakini walidumu katika kumuamini Mungu. Baada ya muda ndio Mungu akaanza kumfungulia milango ya kihuduma na kifedha, akafunguliwa mlango wa kufaa sana katika nchi za jirani kama Kenya na UGANDA ambapo katika mikutano yake Mungu alimuinulia watu wa kusuport. Sasa wale wachungaji waliokimbia vita vya tohara baada ya kurudi na kukuta mwenzao alivumilia mateso na hakumkana Yesu wala kuiacha kazi yake ndio wlianza kuleta uvumi na maneno ya kumchafua. Zikaandikwa bbarua zikapigwa sahihi za wachungaji, zikasambazwa makanisa mengi ya Arusha kwmba huyu ndugu ni freemason, anakunywa damu za watu katika kila ajali inayotokea Arusha, wengine wakavuka hadi Kenya na kuongea kuwa akija Kenya anakuwa anaambukiza dhambi kwasababu ana watoto wengi mitaani na ameoa wake mengi, lakini hayo yote hakuyajibu bali alimkabidhi Mungu na Mungu akamjibia. Bado Mungu aliendelea kumfunguliamilango ya nnje ya nchi na kumpa kibari katika nchi kama vile SUDAN na Somalia ambapo amefungua huduma kadhaa huko. Mbali na huduma pia ni mfanya biashara, na mfugaji, na pia ana mashamba yake pamoja na nyumba kadhaa za kifahari. Ila siri ya kupata vyote hivyo ni utoaji, anaamini sana katikakutoa na pia katika kuwaheshimu masihi wa Bwana. Kwa hiyo toka katika jina la bwana mavi enzi hizo akiwa amepigika lakini leo anaitwa Freemason baada ya Mungu kumbariki. Ama kweli kila hatua unayoipiga maishani huwa inaambatana na majina yake. Sasa na mimi nimegundua kuwa hata kutukanwa na kuzushiwa pia ni sehemu ya baraka. 
Tarehe 22/23 Agosti 2015 Apostle Mkalla ambae ni mlezi wa Makamanda wa Yesu atasimama pale Landmark Hotel na kufundisha siri ya kufanikiwa, pamoja na uvumilivu wa kuwashinda waswahili na maneno yao.

Thursday, June 11, 2015

MTUME WA UREJESHO PETER NYAGA ATOA SHILINGI LAKI SABA KAMA SUPORT YAKE KATIKA SEMINA YA MAKAMANDA

Katika semina ya siku mbili ya makamanda wa Yesu inayotazamiwa kufanyika  tarehe 22 hadi 23 Agosti 2015 katika ukumbi wa Landmark Hotel uliopo Ubungo, Riverside, mambo yanaendelea kuwa mazuri. Katika semina hiyo iliyopewa title ya "GROWING WITHOUT GROANING IN LIFE AND MINISTRY" ambayo itawakutanisha waalimu wazuri na wenye viwango vya hali ya juu kwenye maisha na kihuduma kama vile Baba wa washindi Apostle Vincent Mkalla tokea Arusha, Apostle Livingstone Banjagala,  Mtume wa Urejesho Peter Nyaga, pamoja na mwalimu Stephen Haule, mbali na kuwa mmoja miongoni mwa waalimu lakini Mtume Nyaga ameamua kupanda mbegu yake na kudhamini semina hiyo kwa kutengeneza matangazo yenye gharama ya shilingi laki saba za kitanzania. Kwa niaba ya makamanda wa Yesu, General Comandoo Mtume Kijana Bashando ametoa shukrani zake za dhati kwa Mtume wa urejesho Peter Nyaga kwa kujitoa kwake. Lakini pia amewashukuru waalimu wote waliokubali kushiriki katika semina hiyo na kufundisha watanzania watakaobahatika kuhudhuria kwenye semina hiyo. "Mungu ambariki sana Peter Nyaga na wengine wote wanaotoa suport kwa ajili ya kuwezesha siku hizi muhimu sana ambazo naamini zitakwenda kuwabadirisha watu wengi" alisema Bashando. Kama una biashara au kampuni na ungependa na wewe kuwa mdhaminimmoja wapo katika semina hii unaweza kuwasiliana nasi kupitia simu namba +255713700627l, +255763788459 au kwa email bashandomarwa@gmail.com

Tuesday, June 9, 2015

SIKU MBILI ZA MAKAMANDA NDANI YA JIJI LA DAR ES SALAAM ZINAZIDI KUVUMA NA KUTIKISA AKILI ZA WENGI

Semina ya siku mbili inayotazamiwa kufanyika tarehe 22 hadi 23 Agost 2015 katika Ukumbi wa LandMark Hotel, Dar es salaam, Ni semina ambayo awali ilijulikana kama semina ya From receiving to giving lakini kwa sasa imebadirika na kuwa semina ya Growing Without Groaning in Life &Ministry. Ni semina ambayo watumishi wanne watasimama kwenye madhabahu moja katika nyakati tofauti tofauti, Wanenaji katika semina hiyo ni Founder wa huduma ya Victory Faith Tanzania Apostle Vincent Mkalla toka Arusha, Mtume Wa Urejesho Peter Nyaga tokea RGC Miracle Centre Tabata  Chang'ombe, Apostle Livingstone Banjagala wa Citty Harvest International Church Dar Es Salaam, Pamoja na Mwalimu Steven Haule country Manager wa Letshego Tanzania Limited na pia MD wa Chama cha kusaidiana cha wafanyakazi wa Tegeta,  hawa wote ni waalimu wazuri sana katika maisha na mambo ya kiroho pia hivyo natarajia mabadiriko makubwa sana kwa wale watakaohudhuria katika semina hii. Waimbaji watakaohudumu katika semina hii ni Tumaini Njole, Kuyokwa Mary, Veejay Shwarikuu, King David, Stella Swai, Elandre, Baba Sam, Gastor Sapula, Kuhani Zangina, na wengine wengii. Praise and worship itaongozwa na Bishop Nickodemus Shaboka Jr pamoja na team yake. Hii sio ya kukosa maana watumishi wengi watakuwepo katika semina hii..

Monday, June 8, 2015

MWALIMU STEVEN HAULE ATASIMAMA KATIKA SEMINA YA MAKAMANDA WA YESU NA KUSHIRIKISHA UZOEFU WAKE WA KIKAZI.

Watanzania wengi wamejijenga katika mfumo wa kupokea na sio mfumo wa kutoa. Unakuta mtu anapanga mipango mikubwa huku akitegemea mipango yake ifanikiwe kupitia kipato cha mwenzake. Ndio maana unaweza kukuta mtu anapanga kuoa na kwenye bajeti ya ndoa yake anaweka gharama ya milioni zaidi ya ishirini wakati yeye mfukoni ana shilingi laki moja tu. Sasa hii sio tabia nzuri kabisa, na hii ndio inasababisha nchi yetu iitwe nchi masikini na wakati rasilimali zetu zinaturuhusu kuwa matajiri. Sasa umefika wakati wa sisi kwa sisi kuambiana ukweli kuwa tuondoke katika mfumo wa kutegemea kupokea na tuingie katika mfumo wa kusuport. Hili ndio dhumuni la semina ya Makamanda Wa Yesu ya From receiving to giving, hauwezi ukasuport kama hauna kitu,na ili upate kitu cha kusuport ni lazima ufanye kazi kwa bidii, ndio maana hata Apostle Paul akasema kuanzia sasa mwizi asiibe tena, bali ni vyema akajishughulisha kwa bidii ili apate kiasi kidogo cha kumgawia muhitaji. Semina hii itafanyikia Landmark Hotel tar 22/23 Agost 2015.
Mmoja wa waalimu katika semina hiyo ni Mwalimu Stephen Haule ambae amekuwa na sifa ya kuwa mfanyakazi bora katika kila sehemu anayokwenda kufanyia kazi. Amekuwa mwalimu wa secondary kwa takribani miaka kumi katika shule ya Tegeta secondary, na alianza katika ualimu katika ngazi ya kawaida tu, lakini kadiri siku zilivyozidi kwenda ndipo wakubwa waliziona juhudi zake na kuanza kumpandisha daraja taratibu, hadi anaondoka shuleni hapo na kuhamia katika ajira nyingine wanafunzi wa Tegeta secondary waligoma na wakasema wanamuhitaji mwalimu wao arudi, jambo lililofanya wakubwa wa shule hiyo wamuombe arudi hata kwa masharti ya kumuongezea mshahara anaoutaka ili tu wanafunzi wake wawe na amani.
Katika kazi nyingine aliyohamia aliingia kama mfanyakazi wa kawaida tu lakini kadiri siku zilivyozidi kwenda viongozi waliona juhudi zake na moyo wa kupenda kazi  na wakaanza kumpandisha vyeo taratibu, hadi leo hii amefikia nafasi ya country manager katika kampuni ya Letshego Tanzania Limited. Anamuamini sana Mungu, lakini pia anaamini katika kufanya kazi kwa bidii na katika kuwasaidia wengine ili watimize ndoto zao. Kitu kikubwa ambacho hakipendi  ni hapendi watu wasiojishughulisha na kuamini kila kitu kwao kuwa hakiwezekani, bali anapenda na pia anajitahidikwa kadiri anavyopata nafasi kumsababisha mtu aweze kusimama na kujisimamia maisha yake mwenyewe pasipo kuwa tegemezi wa mtu mwingine.
Ninayo mengi tu ya kumsimulia huyu mwalimu Haule ambae kwa sasa ni miongoni mwa viongozi wanaosimamia chama cha  kusaidiana cha wafanyakazi wa tegeta CHAKUTE, na pia bado ni country manager wa kampuni ya Letshego Tanzania Limited, na pia ni mkufunzi wa mafunzo mbalimbali ya kazi pamoja na ujasiriamali. Binafsi huwa namshukuru na nitazidi kumshukuru kwasababu yeye pia ni mtu aliyeweka alama maishani kwangu, ukitaka kujua mengi kuhusu yeye hakikisha unatuhudhuria semina hii ambayo iko mbele yetu.
Mwalimu Stephen Haule alipokuwa katika ziara ya kikazi Africa ya kusini

Saturday, June 6, 2015

MCHUNGAJI GABRIEL ARUDI KUWASHUKURU MAKAMANDA BAADA YA MUNGU KUWATUMIA KUGUSA MAISHA YAKE KWA NAMNA MOJA AU NYINGINE

Mchungaji Gabriel Y Kalima ametoa shukrani zake za dhati kwa makamanda wa Yesu. Huyu ni Mchungaji ambae takribani mwezi mzima uliopita nilimleta mbele zenu na kuwaeleza juu ya uhitaji wake. Nakumbuka alikuwa anahitaji mtaji wa shilingi laki nne kwa ajili ya kufanya biashara ambayo ingemuwezesha kupata mahitaji yake ya kila siku, na pesa aliyokuwa anaihitaji ni shilingi laki nne tu. Namshukuru Mungu kwa ajili ya wote mliojitoa kwa kuongea maneno ya kutia moyo, lakini zaidi namshukuru sana Apostle Vincent Mkalla ambae aliitoa pesa hiyo yote na kunikabidhi kisha mimi nikamfikishia Mchungaji. Badala ya kufanya biashara ya mabanzi Mchungaji Gabriel ameamua kufanya biashara ya kununua nguo na kuziuza mkoani ambapo biashara hiyo ameikabidhi kwa mama Mchungaji na hivi sasa inaenda vizuri. Siku tano zilizopita Mchungaji Gabriel amekuja ofisini kwangu Chalinze na kunipa shukrani zake za dhati kwa niaba ya makamanda wote, na vilevile nikampa muariko wa kuhudhuria semina ya siku mbili ya makamanda ambayo itafanyika tarehe 22/23 Agosti 2015, Mchungaji Gabriel ameahidi kuwepo katika semina hiyo na amesema atatoa ushuhuda wa jinsi Mungu alivyomtendea kupitia huduma hii ya Makamanda Wa Yesu.
Mchungaji Gabriel Kalima akiwa namke wake.

Friday, April 24, 2015

MUME APOTEZA MAUMBILE YAKE YA KUJIDAI BAADA YA KUTALIKIANA NA MEWE


KUTANA NA KIJANA MOSES N NDOMBA KIJANA ALIYEKITAMBUA KIPAJI CHAKE NA HIVI SASA ANAISHI MAISHA MAZURI KUPITIA HICHO.

Anajulikana kwa jina la Moses Ndomba, mwenyeji wa Songea Ruvuma, ambae tangu akiwa shule ya msingi alipenda sana kujihusisha na michezo ya sarakasi. Mwanzoni alipenda kuifanya michezo hiyo kama sehemu ya kujifurahisha huku akiwa hana mikakati yeyote ya kukiendeleza kipaji chake, lakini alipokuwa akionekana anaruka sarakasi mbele za watu, wengi walimsifia na kumtia moyo kuwa anaweza wakiwemo waalimu wake wa shule ya msingi. Aliendelea na elimu yake ya msingi huko mkoani Songea ambapo pia katika maonyesho ya shuleni alishiriki michezo ya sarakasi. Alipofika darasa la sita kaka yake ambae walikuwa wakishirikiana kwenye michezo alimshauri  wahame kutoka songea na kuja dar ambapo kuna fursa kubwa ya kuendeleza vipaji vyao, kweli Moses na kaka yake walihama kutoka songea na kuja dar es salaam ambapo alimalizia elimu yake ya msingi katika shule ya buguruni A. Baada ya kumaliza elimu yake aliendelea na sanaa yake huku ikizidi kumtambulisha kwa watu mbalimbali na kumfanya apate miariko kadha wa kadha katika harusi na sehemu mbalimbali, mwisho wa siku wakajitokeza watu wa kumdhamini na hatimaye sanaa ya sarakasi ikawa ajira kwake, ya kumuendeshea maisha na kumpa mahitaji ya kila siku. Mwaka jana mwishoni Mungu alimfungulia mlango wa kupata mkataba wa kufanya kazi India kwa mwaka mzima ambapo sasa ameshatimiza miezi minne. Moses anamshukuru sana Mungu kwa hatua hii aliyopiga ambapo anasema ameanza kuona dalili kubwa za mafanikio kupitia sanaa yake, ambapo hadi sasa tayari anamiliki viwanja kadhaa Dae es Salaam na Ruvuma, na mbali na hayo anaamini mambo makubwa sana yataendelea kumtokea maishani mwake. Habari njema ni kwamba Moses ameokoka na anampenda Yesu, na ndoto zake ni kumtangaza Kristo kupitia sanaa yake popote pale anapopata nafasi.. Blog ya makamanda inamtakia mafanikio zaidi Mr Mosses Ndomba

Add caption




Wednesday, April 22, 2015

ZITAMBUE AINA TATU ZA WANADAMU NI SOMO LINALOFUNDISHWA NA MTUMISHI WA MUNGU MCHUNGAJI PASCAL LINUS MJILI, JITAHIDI USOME HADI MWISHO ILI UJITAMBUE UKO KWENYE KUNDI GANI

SOMO: AINA TATU 3 ZA WANADAM.
Ktk ulimwengu huu tuonaishi kumejaa Wanadam wenye mitazmo mbalimbali tamaduni na desturi tofauti. Ktk some hili nitazungumzia aina Tatu za Wanadam ambazo zitatusaidia kujitasmini na kujitambua kuwa uko ktk kundi au group gani. Natumaini kila mmoja wetu atapa fursa ya kujifunza ktk some hili.
1. MWANADA WA ASILI(Natural person)
Ni mtu ambaye huishi kwa kufuata mifumo ya maisha ya kidunia. Ni mtu ambaye hajaokoka (ungenerated person) Ni mtu asiyemjua Mungu, hana ushirika wala mawasiliano na Mungu. Ni mtu aliyekufa kiroho, (spiritual dead person ) he is under control of Satan. Things of God are foolishness to him. Hijivunia dini zilizoanzishwa na wanadam badala ya wokovu ulioletwa na Yesu KRISTO. Fikra na akili zao zimetiwa Giza, mioyo yao imekufa ganzi, wana mioyo migumu wamefakana na uzima wa Mungu (Efeso 4:18-19) Hekima yao ni upuuzi kwa Mungu na Hekima ya Mungu ni upuuzi kwao.
2.MTU WA KIROHO (spiritual person)
Ni mtu alilye okoka (regenerated person) amezaliwa mara ya pili. Mungu Baba mwana na Roho mtakatifu wanakaa ndani yake. Ana ushirika na mawasiliano na Mungu wa milele. They can understand spiritual things because they are no longer natural person, they are converted from natural to spiritual. Wako tayari kutii na kufuata maelekezo ya Mungu, Neno na watumishi wake. Niwanyenyekevu..........
Niwatakatifu wameoshwa dhambi na ndiyo ambao Mungu wa mbinguni anajivunia (Zaburi 16;3) Ni watu ambao wana sifa kuu 2
(A) Makuhani
(B) Wafalme Ufunuo 5:10. Ni makuhani juu ya maisha yao wenyewe maanake waweza kujiwakilisha (kujiombea) kwa Mungu kwa njia ya damu ya Yesu KRISTO. Pia wanauwezo wa kuwaombea wengine na wakasikilizwa (YOHANA 9:31
Ni watawala juu ya nchi, uchumi, biashara makampuni mf ni Yusufu aliye tawala misri. Wana nguvu juu ya Mapepo majina uchawi. Wana amri juu Magonjwa yote na udhaifu wa kila aina.
3. MTU WA MWILINI (Carnal person )
Ni mtu aliye zaliwa mara ya pili ila hajakuwa kiroho, tabia za mwili huchukuwa sehemu kubwa ya maisha yake (1Kor.3:1-3) watu hawa wapo makanisa ya watu waliozaliwa mara ya pili ila tabia zao ni za kimwili mf. Mashindano, chuki, fitina, wivu na mengine kama hayo. Ni watu ambao wana moyo mapacha yaani moyo uliogawanyika.
Wanapenda vya dunia na vya Yesu pia wanavitaka . (they are mr&mrs both ways. They are still dancing and controls awith the devil. They always compromising with the world. Eliya alwahi kukutana na aina hii ya wayahudi ambao mioyo yao ilimwabudu Baali na bado wakitaka kuitwa watu wa Mungu wa Israel. Eliya aliwambia mtasitasita kati ya mawazo na njia mbili hata lini!? Baali akiwa ni Mungu mfuateni au BWANA akiwa ndiye Mungu haya mfuateni yeye.
Natumaini mpendwa umejifunza na kujitathimini uko ktk kundi gani ktk haya matatu. Fanya maamuzi ya kuwa ktk kundi la mtu wa kiroho.
Kama uko ktk kundi la mtu wa ASILI basi tubu dhambi na kuziacha mwamini Yesu ili uzaliwe mara ya pili, nawe utakuwa mtu wa kiroho.
Kama umeokoka lakini bado unatabia za kimwili Yesu KRISTO unampenda lakini duniani nako unapenda fanya maamuzi leo ya kuwa mtu wa kiroho. Huwezi kupanda mabasi au ndege mbili ktk safari moja. Tumia basi moja au ndege moja kwa safari moja. Kwa maana mtu akiipenda dunia kumpenda Mungu hakumo ndani ya . yake. (1 YOHANA 2;15
Asanteni kwa kunisikiliza
Pastor Pascal Linus Mjili

Tuesday, April 21, 2015

MBUNGE WA MIKUMI ANAESUBILIA KUAPISHWA AUUNGA MKONO MTANDAO WA MAKAMANDA

Mwanamuziki mkongwe na icon of Bongo FlevaProfesor Jay amechangia sadaka ya ujenzi wa kanisa la Neema ya Kitume. Mwanamuziki huyo ambae kwasasa ametangaza nia ya kugombea ubunge baada ya wananchi wa Morogoro, jimbo la mikumi kumuhitaji ameongea na blog ya makamanda na kusema kuwa siku zote moyo wake huwa anahamisika sana kusaidia kazi yeyote inayomuhusu Mungu. "Niliona Tangazo lako facebook la kuchangisha pesa kwa ajili ya ujenzi wa kanisa na nikahamasika sana kutoa, naomba nitoe kidogo nilicho nacho pamoja na majukumu mengi niliyo nayo lakinini bora nishirikiane nanyikatika baraka hii ya kuijenga nyumba ya Mungu" Maneno hayo aliyasema huku akiambatanisha na pesa ambayo hakupenda sana itajwe kwa kudai kuwa sadaka siku zote ni siri na ametoa kwa ajili ya Mungu na wala sio kwa kutafuta ufahari. Profesa Jay ambae ana sifa ya kuubadilisha muziki wa bongo fleva toka kwenye kudharaulika hadi kugeuka na kuwa ajira kwa vijana wengi amesema hata huku bungeni ninapoelekea naamini Mungu ndio atakaenipa nafasi hiyo ambapo dalili zote nimeanza kuziona. Naomba muwe mnanitembelea hata baada ya kuingia bungeni maana mimi binafsi ninaamini sana katika ushauri wa watu mbalimbali hivyo msiache kunipa mawazo yengu.............. Blog ya makamanda inamshukuru sana Profesa Jay kwa mchango wake lakini pia kwa moyo wake wa kupenda kuwakaribisha wageni nyumbani kwake. Mungu akubariki....
Profesa Jay akisisitiza jambo katika maongezi yake na Kamanda Bashando
Nyumba ya Profesa Jay kwa nnje
Profesa Jay akiwa katika picha ya pamoja na Makamanda
Baadhi ya magari ya Profesa Jay
Profesa jay akizungumza jambo na Kamanda wakati anaondoka




Monday, April 20, 2015

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA




Simu: 255-22-2114 615, 211906-12
Barua pepe: nje@nje.go.tz
Barua pepe: gcu@nje.go.tz
Tovuti : www.foreign.go.tz
Nukushi: 255-22-2116600

20 KIVUKONI FRONT,
P.O. BOX 9000,
11466 DAR ES SALAAM,
Tanzania.


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe, amesema leo kuwa hakuna Mtanzania kati ya watu wanane waliouwawa katika mashambulizi dhidi ya wageni huko Durban na Johannesburg nchini Afrika ya Kusini.
Mhe. Membe amewaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuwa taarifa zilizosambazwa na baadhi ya vyombo vya habari kwamba Watanzania watatu wameuwawa katika mashambulizii hayo siyo za kweli.
"Nimehakikishiwa na Waziri wa Usalama wa Afrika kusini, David Mahlobo, asubuhi hii kuwa hakuna Mtanzania kati ya watu wanane waliouwawa, ambao ni raia wa Ethiopia, Zimbabwe, Malawi na Swaziland," ametaarifu Mhe. Waziri.
Amesema serikali ina taarifa kuwa kuna Watanzania watatu waliofariki dunia nchini Afrika Kusini, lakini hawakuuwawa katika mashambulizi ya wenyeji dhidi ya wageni.
"Watanzania hao ni Rashidi Jumanne, ambaye imetaarifiwa alipigwa risasi katika tukio la ujambazi, kilometa 90 nje ya mji wa Durban; mfungwa Athumani China Mapepe, aliyeripotiwa kuchomwa kisu gerezani wakati wa vurugu za wafungwa, na Ali Heshima Mohamed, ambaye alifariki hospitalini kutokana na ugonjwa wa TB," alieleza Mhe. Membe.

Mwili wa marehemu Mohamed ulirejeshwa nchini jana kwa mazishi. Mhe. Waziri alitaarifu kuwa kuna Watanzania 23 katika kambi iliyotayarishwa na serikali ya Afrika Kusini huko Durban kuhudumia wageni wanaokimbia mashambulizi hayo ya wenyeji, na kuwa utaratibu unafanywa kuwarejesha nyumbani raia 21 walioomba. "Wawili wamesema hawako tayari kurudi."
Mhe. Membe amesema taarifa ya serikali ya Afrika Kusini inaonyesha kuwa hali ya utulivu imerejea Durban na Johannesburg katika saa 48 zilizopita kutokana na juhudi za Rais Jacob Zuma na kamati maalum ya mawaziri aliyoiteua kushughulikia mashambulizi hayo.
Mapema jana, Mhe. Membe alimwita Balozi wa Afrika Kusini nchini Tanzania, Mhe. Thamsanqa Dennis Mseleku,       na kuelezea kukerwa kwa serikali na mauaji ya wageni na akataka hatua madhubuti zichukuliwe kuhakikisha usalama wa Watanzania nchini Afrika Kusini.
Alisema Tanzania inaunga mkono taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe, ambayo imelaani vikali mashambulizi ya Waafrika kutoka nje ya Afrika Kusini. Hata hivyo, Rais Mugabe, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU), amesifia hatua zinazochukuliwa na serikali ya Afrika Kusini kukomesha mashambulizi hayo na kurejesha utulivu.
Mhe. Membe aliwataka Watanzania waishio Afrika Kusini na kwingineko nje ya nchi, kujitambulisha kwenye balozi zetu ili iwe rahisi kufuatilia usalama wao na kuwasaidia pale yatokeapo majanga.
"Hatuna takwimu sahihi za idadi ya Watanzania waishio Afrika kusini kwa sababu wengi wao wamekwenda huko kwa njia za panya," alisema. Inakadiriwa kuna Watanzania 10,000 waishio Johannesburg na Durban. 
Akijibu swali la mwandishi wa habari, Mhe. Membe alisema Tanzania inapaswa kutumia utajiri mkubwa wa gesi asilia ilionao ili kuendeleza viwanda vidogo, vya kati na vikubwa vitakavyotengeneza ajira za kuvutia kwa vijana ili wasikimbilie nchi za nje na kuhatarisha maisha yao.


Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Dar es Salaam
20 Aprili 2015.

Sunday, April 19, 2015

KWAYA YA BUGANDO YASHAURIWA KUWATEMA WANAKWAYA WANAOILETEA SKENDO KWA TABIA ZAO ZA KIPAGANI

Kwaya ya bugando ni kwaya kubwa sana hapa nchini, na ni kwaya iliyopata kibari sana kwa mzee wetu Hayati Moses Kulola. Kila mkutano ambao Askofu Kulola alikwenda kuhudumu ni lazima angeambata na kwaya hii ambayo hata mimi niliposhuhudia mikutano miwili mitatu nilivutiwa sana na uimbaji wao pamoja na staha waliyokuwa nayo. Lakini sasa mambo ni tofauti kabisa, baada ya Askofu Kulola kumaliza kazi yake na kuondoka hivi sasa baadhi ya wanakwayawameota mapembe na kufichua makucha yao, chakushangaza ni watu ambao wameishi kwa Askofu Kulola na wengine kusomeshwa elimu za juu ingawa sio watoto wake wa kuzaa, ila leo hii wamebadirika na wakuwa wa kidigital zaidi. Baadhi ya watu wamekuwa wakikereka na tabia za baadhi ya wanakwaya haoambao wamehudumu kwa muda mrefu na kwaya hiyo, lakini wengie wameishia kuwa walevi na wauza bar, wengine wakiwa na lugha za chafu huku wakisakamwa na skendo za kugombea mabwana. Mmoja kati ya walalamikaji ambae ni jirani wa dada mmoja katika kwaya hiyo, amedai kuwa wapo wanakwaya waliomaanisha lakini pia wako ambao hawajamaanisha ila tuwamejishikiza kwenye injili huku wakingojea mambo yao yaende vizuri watupilie mbali maigizo ya wakovu wanayoyafanya.
Blog ya Makamanda inatoa ushauri kwa msimamizi na mlezi wa kwaya hiyo awe mkali sana kwa wote wanaoonyesha tabia za kuichafua kwaya ambayo inaheshimika sana, ikiwezekana hata awatimue na kubakia na watu waliomaanisha, maana kazi ya Mungu inahitaji kujikana..
Mwanakwaya wa Kwaya ya Bugando akiwa amevalia mavazi ambayo hatuna uhakika kama Askofu Kulola angeyaafiki enzi akiwa hai

Saturday, April 18, 2015

BISHOP NICKODEMUS SHABOKA NA ROSE SHABOKA MUNGU KAWAJAALIA MTOTO WA KIUME

Ni furaha ya ajabu kwa wanandoa wawili Nickodemus pamoja na mkewe Rose Shaboka baada ya Mungu kuwajalia mtoto wa kiume ambae wamempa jina la Prophet JM Shaboka. Baraka hii ilifanyika jana, Bishop Nickodemus amefurahishwa na ujio wa mtoto huyo. Mama wa Mtoto anaendelea vizuri.. Blog ya makamanda pamoja na makamanda wote tunatoa pongezi sana kwa wawili hao na tunazidi kumshukuru Mungu kwa kumsaidia Rose akajifungua salama..


Friday, April 17, 2015

BAADA YA VIPIMO VYA DAKTARI KUONYESHA KUWA EMMANUEL MBASHA HAKUBAKA, SASA MBASHA AIBUKA NA KIBAO KIPYA CHA KUUSHANGILIA USHINDI WA YESU DHIDI YA MAISHA YAKE

Majibu ya daktari yametoka na kuonyesha kuwa Emmanuel Mbasha mume wa Frola Mbasha hakumbaka yule binti anaedaiwa kuwa ni mdogo wake Frola. Majibu hayo ya daktari yamempa furaha sana mume wa mwanamuziki mkubwa wa nyimbo za injili Frola Mbasha, ambae inakaribia mwaka sasa wakiwa wametengana na kila mtu yuko kivyake. Emmanuel Mbasha amesema "Hakika Mungu anaisikia sauti ya wanyonge, mimi nitaendelea kumtumainia yeye, na ninaamini mambo yatakwenda vizuri" Nilipomuuliza sakata la Gwajima na Polisi Mbasha alisema hawezi kuongelea hayo ila anachoweza kusema ni kwamba anawashukuru wale wote wanaomuombea kila siku na kulia pamoja nae katika mapito yake. Mbasha ameishukuru sana blog ya makamanda hususan Mwanaharakati wa ukweli Bashando kwa ushirikiano anaouonyesha kwake. Nawaomba watanzania muipokee kazi hii ambayo naamini itawabariki, na ndani yake nimeimba mambo harisi na kwa hisia kubwa. Nyimbo inaitwa lazima kieleweke, unaweza kuidownload au kuishare kwenye wall yako ili watu wengi wapate ujumbe huuu. Mungu akubariki.

IJUE HUDUMA YA HUDUMA YA VICTORY FAITH ILIYOEGAMIA KATIKA IMANI YENYE MATENDO MAKUU YA KUUTUKUZA UFALME WA MUNGU

Victory Faith ni huduma kubwa iliyoenea Tanzania hadi nnje ya Tanzania, ni kanisa linalosimamiwa na Apostle Vinceent Mkalla ambalo makao yake makuu ni Arusha, Maeneo ya Kijenge juu. Kanisa hili ni moja wapo ya makanisa yenye watu wengi wenye uwezo kiuchumi na wanaojitambua kulingana na mafundisho mbalimbali wanayoyapata kutoka katika madhabahu hiyo. Baada ya kupata habari na sifa kedekede toka kwa watu kuhusiana na kanisa la Victory Faith niliamua kumtafuta Founder wa kanisahilo Apostle Mkalla na kumuuliza maswali mawili matatu. Ndipo nilipotambua huduma hiyo imeanza tangu mwaka 1994, na katika miaka hiyo Mungu alizungumza mambo mengi sana na mtumishi huyu ambae aliyaandika huku akiamini yatakuja kutimia baadae. Apostle Mkalla ambae ni kiongozi mkuu katika kanisa la Victory Faith ambayo kwa kiswahili inamaanisha Imani ya Washindi amesema mafanikio ya huduma yake hayatokei kwa bahati mbaya bali ni mipango ambayo Mungu alimletea kwa njia ya maono na akaamini na kuyasimamia hadi leo hii yamekuwa katika matendo na yanaonekana. Miaka 20 iliyopita Mungu alimuonyesha aina ya jengo zuri sana atakalomjengea kwa ajili ya watu waake kuabudia, na yeye akaandika na baada ya kuandikika akachora ramani na kutengeneza kibanda kidogo chenye mfano wa kanisa ambalo Mungu alimuonyesha kwenye maono, na akavihifadhi, lakini leo hii yametimia na ameshajenga makanisa mengi sana nchini na nje ya nchi. "Namshukuru sana Mungu ametuwezesha ujenzi ambao tarehe 01/july/ tutakuwa tunafikisha mwaka mmoja. Tumenunu plot hapa mjini kwa bei ya shilingi miliion190/- na Tumejenga jengo lenye mfumo wa kisasa wa Inter net. Ac camera za usalama na za video. Sounding Cable nk Jengo hili lina office12, kwa ajili ya idara zote. Na pesa zote tumezitoa mfukoni mwetu na kwa umoja wetu wala hatujasaidiwa na wadhamini au wanasiasa" Akiendelea kuongea na blog ya Makamanda Apostle Mkalla amesema kuwa anamuamini Mungu katika utoshelevu wote, na pia ukiwa na Mungu unakuwa na utajiri wote pamoja na baraka zote. Kanisa hili limejengwa kwa muda wa miezi tisa na sasa linaelekea ukingoni................................................
Apostle Mkalla ambae anaamini katika kuhubili injili ya kifalme amesema anapenda sana kuonyesha ubora katika kazi ya Mungu na ndio maana yeye hakubali kulala katika nyumba nzuri na kuiacha nyumba ya Mungu katika hali mbaya, nyonge na dhaifu. Japo kuna mapito mengi sana amepitia lakini katika yote ameshukuru sana Mke wake Glagys Mkalla ambae yeye amempa jina la  The Machine, kwa jinsi anavyomuombea na kumtia moyo kwenye kazi ya Mungu, lakini pia kwa kuiongoza vyema team ya The Arrows ya kanisani hapo kwenye maombi. Apostle Mkalla amewashukuru sana pia na wachungaji wanaoongoza makanisa mengine ya Victory Faith hapa Tanzania na nnje ya Tanzania pamoja na waumini wote ambao wanatumika nae katika roho moja na nia moja. Kwa leo nimekuletea haya lakini bado nina mengi zaidi nitaendelea kukudokeza 
Mama Mchungaji Gladys Mkalla


Apostle Vincent Mkalla akiwa na Mke wake Glayds Mkalla madhabahuni
Mfano wa jengo la kanisa ambalo Apostle Vincent aliutengeneza kwa ghalama zake baada ya Mungu kumuonyesha jengo hilo kwenye maono
Kanisa la Victory Faith kwa muonekano wa mbele
Kanisa la Victory Faith kwa nnje
Waumini wa kanisa la Victory Faith wakiendelea na ibada
Ramani ambayo Apostle aliichora baada ya kupata maono
Picha ya kanisa la victory Faith
Ujenzi wa kanisa ukiwa unaendelea





Thursday, April 16, 2015

MWANAHARAKATI WA UKWELI BASHANDO AMUULIZA MASWALI MACHACHE FADHER NKWELA

Katika utoto wangu na hadi sasa ni kijana ninaeuelekea utu uzima nimekuwa nikisikia sana jina la Father Nkwella likitajwa na watu wengi, wakatoliki na na wakristo wasio wakatoliki. Wapo waliomuongelea kwa uzuri na wengine kumuongelea kwa ubaya, lakini katika miaka yote sijawahi kubahatia kumuona live Father Nkwella na hata kanisa lake sijui liko sehemu gani. Kwa bahati mbaya nilipata msiba siku ya ijumaa ambapo mazishi yalifanyika siku ya jumanne ya tar 12/April/2015 ambapo katika msiba huo Father Nkwella alihudhuria kwasababu marehemu alikuwa ni rafiki yake wa karibu sana na muumini wake. Baada ya mazishi kufanyika kuna mtu alinishtua kuwa yule unaemuona mbele yetu unamjua? Nikamjibu simfahamu, akaniambia kama umewahi kusikia mtumishi anaeitwa Father Nkwella ndio huyo. Aliponiambia hivyo nikasema siwezi kuondoka na kuishia kumuona kwa mbali ngoja nikamuombe angarau nipige nae picha, ingawa alikuwa amezungukwa na watu wengi lakini nilifanikiwa kupenya na kumfikia, nikakaa pembeni yake kwa muda wa dakika 10 na alipomaliza kuongea na watu ndio nikamumpa mkono na kumsalimia. Alipoitikia salamu yangu nikaonyesha jinsi nilivyofurahi kuonana nae na nikamuomba kupiga nae picha, hakuonyesha kusita akakubali mara moja, wakati tumemaliza kupiga picha niamuuliza kwa sauti ya chini chini, "Kanisa lako kwa chalinze liko wapi? Akanijibu hana tawi chalinze ila taratibu taratibu tu mambo yatakuwa. Nikamuuliza tena kwanini watu hasa jamii ya wakatoliki wenzake wanamuongelea vibaya na kufikia hadi hatua ya kuwanyima sakramenti waumini wake? Akanijibu, huduma yeyote ya kweli lazima ikutane na vita pamoja na kukataliwa na hiyo ndio tafsiri sahihi ya kukinywea kikombe cha Kristo.  Swali la mwisho nikamuuliza je, yeye anatofauti gani na wakristo waliookoka? Na kwanini asijiite mchungaji yeye anajiita Father? Akanijibu eneo tulilopo sio sahihi sana kwa kujadiri mambo hayo ila nikihitaji kujua mengi ananikaribisha kanisani ubungo. Baada ya kunijibu hayo kwa njia ya hekima na upole kabisa niliona kweli nimuache kwanza mzee aendelee na majukumu mengine lakini nimepanga kumtafuta ili nimuulize mambo mengi sana kuhusiana na huduma yake.
Father Nkwella akiwa anapeana mkono wa salamu na Mjane wa Marehemu
Father Nkwella akizungumza na Mjane wa Marehemu
Father Nkwella akiwa amezungukwa na familia ya marehemu

MTAKATIFU NA UZIDI KUJITAKASA MAANA KAMA IMANI NDIO IMEFIKIA HAPA BASI INAONYESHA ULE MWISHO UKO KARIBU

Mtumishi wa kike akimfanyia maombi ya ulinzi mwanaume mmoja mchana kweupee huku wote wakiwa hawana nguo, sijui fomula hii wameitoa wapi lakini ni imani yao na maneno yao yanaonyesha kuwa hawa ni wakristo na hapo walipo wanadhania kuwa wamejaa roho. Sina uhakika kama ni ufunuo bali ninaamini huu ni ukengeufu wa kiimani unaotokana na kupata fundisho baya toka katika kanisa au dini fulani yenye mafunuo funuo masauti sauti hivii. Hebu itazame hii.

Wednesday, April 15, 2015

JINYAKULIE BARAKA ZAKO KWA KUCHANGIA UJENZI WA NYUMBA YA IBADA

Kanisa la Neema Ya Kitume. (A,M.G) lililopo tabata linanaendelea na shuguli ya ujenzi.. Kanisa hilo ambalo linasimamiwa na Apostle Bethania Simon liko katika uhitaji wa vifaa mbalimbali vya ujenzi ambavyo vitafanikisha kumalizika kwa kanisa hilo. Blog ya makamanda ilipozungumza na Apostle Bethania tulimuuliza ni hatua gani waliyoifikia kwenye ujenzi wa jengo hilo, Apostle Bethania alisema anashukuru kwasababu hadi hapo walipofika wameshapiga hatua, na sehemu iliyobakia ni ndogo sana ukilinganisha na walipotoka. "Kwa sasa tunahitaji mifuko 30 ya simenti pamoja na mabati 70, tunamshukuru Mungu kwa kutuinulia watu mbalimbali ambao wanajitokeza kuisuport kazi ya Mungu" alisema Apostle Bethania, akiendelea kuongea alitoa shukrani zake kwa mzee mmoja aliyemtaja kama MR SAMSON MAGOTI aliyeahidi kutoa mabati 60 kwa ajili ya ujenzi wa kanisa hilo, lakini amesema bado ana uhitaji wa mabati 70 maana ili jengo likamilike yanahitajika mabati 130. Blog ya makamanda inakuletea ombi hili na kukushauri uchangie kwa chochote ulicho nacho na Mungu wa mbinguni atakujaza na kukuongezea pale ulipopunguza.
Kwa uliyeguswa na kusuport kazi hii unaweza kutuma pesa yako kwa Mpesa 0755 259780 au tigopesa 0715 796667 Au kama unaweza kununua vifaa kwa jinsi vilivyo unaweza kuwasiliana na Apostle Bthania kwa namba hizo zote mbili...
Apostle Bethania Simon akisaidia kufanya kazi katika ujenzi wa nyumba ya BWANA
Waumini wa kanisa la neema ya kitume wakiendelea na kazi ya ujenzi